Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) kwa kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali kutoa maoni yao kuhusu ombi la marekebisho ya bei za majisafi na usafi wa mazingira za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA), 22 Agosti 2023.

 

Pongezi hizo zilitolewa kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude, aliyemuwakilisha RC huyo na kueleza kuwa, EWURA inastahili kupongezwa kwa kuendelea kusimamia na kutekeleza sera ya uwazi kwa vitendo.

 

kwa niba ya RC Shinyanga nawasilisha pongezi kwenu EWURA kwa kuendelea kuwashirikisha wananchi kutoa uamuzi wa mustakabali wa maisha yao ya kila siku”. Alisema Mkude

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. George Mhina alisema, uwazi ni moja ya nguzo ya maadili ya EWURA hivyo Mamlaka itaendelea kuzingatia suala hilo katika utekelezaji wa majukumu yake.

 

Mkurugezi Mtedaji wa SHUWASA Mha.Yusuph Katopola, ameeleza kuwa, ombi la kurekebisha bei za maji na usafi wa mazingira ni kwa kipindi cha miaka mitatu yaani 2023/4; 2024/25 na 2025/26; likianisha kuongezeka kwa gharama za huduma kwa wastani wa asilimia 47.

 

Mkurugenzi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhendisi Yusuph Katopola akiwasilisha mapendekezo ya bei za maji kwa wadau  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa EWURA kanda ya ziwa  George Mhina akizungumza kwenye taftishi iliyolenga kupokea ombi la kurekebisha bei za maji kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkunde awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, uliolenga kupokea mapendekezo ya bei mpya za maji  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la serikali (GCC) Mr. Julius Mwambaso akitoa ushauri kwenye mkutano huo  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi kutoka Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na Maji EWURA CCC Bwana Joseph Ndatala akitoa ushauri kwenye mkutano huo  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa mikutano jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga.

 

Mkutano ukiendelea  Jumanne Agosti 22,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga 






Share To:

Misalaba

Post A Comment: