Mratibu wa Ufuatiliaji moto kwa njia ya satellite TFS Kekilia Kabalimu, akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, maelezo juu ya kitengo hicho kinavyofanya kazi zake, wakati alipolitembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, sehemu ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania leo Agosti 04, 2023 kwenye Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo yanafanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Kelilia alisema utambuzi na ufuatiliaji wa moto kwa njia ya mtandao unasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa misitu kwa urahisi kutokana na kuwepo kwa taarifa ya tahadhari ya mpema juu ya uwepo wa moto, hali ambayo inasaidia kujiweka tayari kuudhibiti moto kwa haraka zaidi.
Akizungumza mara baada ya kupata maelezo hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas aliipongeza TFS kwa kutumia tekinolojia ya kisasa kukabiliana na masulaa ya moto nchini lakini alitoa wito wa kueneza elimu hio kwa wananchi.
“Toeni elimu hii nzuri ya kukabiliana na majanga ya moto kwa wananchi ili wakaweze kupata uelewa mzuri wa namna ya kutambua , kufuatilia na kudhibiti mioto inayochomwa sana kwenye misitu ya hifadhi ili kuepuka madhara makubwa ya kuharibu misitu nchini” alisema Kanali Thomas.
Post A Comment: