Na John Walter-Manyara

Katika kuendeleza Michezo nchini, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amezitaka sekta binafsi kutumia faida wanazozipata kuwekeza katika tasnia ya michezo.

Ametoa  wito huo leo Agosti 6,2023 kwenye sherehe za siku ya Simba (SIMBA DAY) inayofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Mgeni Rasmi amekuwa mgeni rasmi katika tamasha  hilo la Simba SC ambapo pia ameupongeza uongozi wa timu hiyo kwa kupandisha kibegi chenye jezi mpya  mlima Kilimanjaro na kusema kitendo hicho kimetangaza utalii wa nchi.

Tamasha hilo  limehudhuriwa na maelfu ya Mashabiki wa Simba na viongozi mbalimbali wakiwa wameujaza uwanja huo mkubwa nchini (FULL HOUSE).


Share To:

Post A Comment: