RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na
mabadiliko yanayoendelea Bohari ya Dawa ( MSD) na kuwataka waendeleee kuchapa
kazi.
Rais Samia amesema hayo Jumamosi Agosti 19,
2023 jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na taasisi
za umma.
Rais Dk.Samia akiwa amemsimamisha Mkurugenzi wa
MSD, Mavere Tukai alisema taasisi hiyo ni kati ya mashirika yaliyo badilika na
matumaini yake itakwenda kufanya vizuri hasa katika mfumo wa uuzaji wa Dawa Afrika kwa kuwa na soko kubwa
hususani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).
Post A Comment: