Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umeshiriki na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa washiriki wa kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma, linaloendelea jijini Tanga. 

Meneja waNSSF Rehema Chuma alikuwa miongoni mwa waliotoa mada katika kongamano hilo lililoanza tarehe 23 Agosti, 2023, amesema kupitia kongamano hilo NSSF imetoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ambayo imebeba kundi kubwa kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote ili waweze kujiunga na kuchangia katika Mfuko kwa maisha yao ya sasa na baadaye.

Lengo la kongamano hilo ni kueleza fursa za biashara zinazoambatana na mradi wa bomba la mafuta Afrika Mashariki (EACOP) hivyo mradi huo ni fursa kwa NSSF kupata wanachama wapya ambao watapata ajira za moja kwa moja na wale watakaonufaika na ajira za muda pamoja na wanufaika wengine kama vile mama lishe na bodaboda ambao wataweza kujiunga na kuchangia katika Mfuko.

Meneja huyo aliwahamasisha wanawake kuchangamkia fursa za mradi wa bomba la mafuta na pia amewataka kujiunga na kuchangia katika Mfuko ili waweze kujiwekea akiba yao ya sasa na baadaye.

Katika kongamano hilo, NSSF licha ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii pia itaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana zikiwemo za nyumba na viwanja ambazo zinauzwa kwa bei nafuu
 
 
Mmoja wa washiriki wa kongamano la wanawake (Daraja Comference )lililofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera akipata elimu ya uifadhi wa jamii kutoka kwa meneja wa NSSF Rehema Chuma mara baada alipotembelea katika banda la mfuko huo.
Meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Rehema Chuma(kushoto)  akiwa katika kongamano la Daraja Comference lililoandaliwa na mbunge wa mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge ,ambalo limewakutanisha wanawake zaidi ya 1000 wa mkoa wa Tanga kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi.
Share To:

Post A Comment: