Na; Moreen Rojas, Dodoma.
Hadi kufikia mwezi Juni 2023, jumla ya ajira 145,245 zimezalishwa kwa Watanzania kupitia miradi mbalimbali ya uwekezaji ambapo wanawake ni 29,049 (20%) na wanaume 116,196 (80%).
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi.Being'i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa vipaumbele vya baraza hilo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Aidha amesema kuwa jumla ya makampuni ya Kitanzania 2, 010 yamenufaika kwa kupata kazi mbalimbali katika miradi inayosimamiwa na kuratibiwa na Baraza.
"Mafanikio katika kuendeleza viwanda vidogo na kati (SANVN Viwanda Scheme)*: Lengo kubwa ni kutoa fursa kwa Watanzania kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, kupata mikopo yenye riba nafuu hususan kwa viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo" Amesema Bi.Issa
Aidha ameongeza kuwa hadi Juni 2023 mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.8 ilitolewa kwa miradi 65 katika mikoa 13 nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma za kuwawezesha wananchi kiuchumi zinapatikana karibu na wananchi pia kupatikana katika sehemu moja inayotoa mikopo, mafunzo, urasimishaji wa biashara, ujuzi kwa wafanyabiashara, uongezaji thamani ya mazao, elimu ya kodi na upatikanaji wa masoko.
"Hadi Machi, 2023 jumla ya vituo vya uwezeshaji 18 vimeanzishwa katika mikoa 6 ya Shinyanga (Vituo 2), Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma (Vituo 6) na Dodoma (Vituo 7), Vituo viwili (Morogoro na Pwani) viko kwenye hatua za kuongeza huduma wezeshi na kuweza kuwa vituo vya uwezeshaji kamili kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017nchini"Amesisitiza Bi Issa
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 vituo vya uwezeshaji vimetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 9.4 kwa wajasiriamali 4,017nchini.
" Imeanzishwa kanzi data ya Taifa ya uwezeshaji ambayo lengo kuu ni kuwaunganisha wawekezaji na watoa huduma mbalimbali za biashara. Hadi kufikia mwezi Juni 2023 jumla ya watoa huduma 186 na Wawekezaji 17 walikuwa wamesajiliwa"
"Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni majukwaa ambayo yako mikoa yote 26 nchini kwa ajili ya kukutana na kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo mafunzo ya kujengewa uwezo katika shughuli zao za kujiongezea kipato"
Kwa upande wake msemaji mkuu wa serikali Ndugu Gerson Msigwa amewataka watanzania kuacha kupenda njia za mkato na kwenda kwenye taasisi za mikopo zinazojulikana na serikali.
"Hakuna mkopo wa harakaharaka mtandaoni,watanzania wenzangu achaneni na matapeli wa mitandaoni"Amesisitiza Ndg.Msigwa
Aidha amewasihi watanzania mikopo yote inapitia kwenye ngazi za halmashauri watanzania wafuate taratibu zote ili kuepuka kutapeliwa hasa mikopo inayotangazwa mitandaoni.
Post A Comment: