Naibu Waziri wa Maji Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea na kukagua utekeleza mradi wa ujenzi wa Bwawa la kidunda unaogharimu shilingi Bilioni 329.47 .
Mhe. Mahundi amesema kuwa Mradi huo ni wa kimkakati wenye lengo la kuhakikisha maji yanapatikana katika kipindi chote cha mwaka katika mto ruvu ambao ni chanzo kikuu cha maji jiji Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya mkoa wa pwani ili kukabiliana na changamoto ya ukame ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara na kusababisha upungufu mkubwa wa maji.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw.Kiula Kingu ameeleza kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa Bwawa la kuhifadhi maji lenye mita za ujanzo milioni 190; Ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 20; ujenzi wa njia ya msongo mkubwa wa umeme kutoka kidunda hadi chalinze umbali wa kilomita 101; na ujenzi wa barabara ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi kidunda. Hadi sasa Mkandarasi wa ujenzi na mtaalam Mshauri atakayesimamia ujenzi ameshapatikana na shilingi Bilioni 49.4 ambazo ni fedha za ndani zimetolewa ikiwa ni malipo ya awali ili kuanza ujenzi wa bwawa hilo.
Post A Comment: