Leo Agosti 11, 2023 Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa atashiriki katika hafla fupi ya kuwaaga wachimbaji 200 wa Madini, Wafanyabiashara wa Madini, Watoa huduma Migodini, Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini (FEMATA), Viongozi wa Wizara ya Madini na Watendaji wa Taasisi zake wanaotarajia kusafiri kuelekea nchini China
Ziara hiyo nchini humo imelenga kukutana na wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini China, kutembelea Viwanda vya kutengeneza mitambo na vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji wa Madini, kupata uzoefu wa wafanyabiashara wa Madini waliopo China na kupata teknolojia za uchimbaji na uchenjuaji.
Hafla hiyo ya kuwaaga itafanyika katika Ukumbi wa Soko la Madini jijini Dar es Salaam
Taarifa rasmi itawasilishwa
Post A Comment: