Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi(Mb) amefanya ziara ya kikazi Wilayani Mafia kwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya Jibondo, Kilindoni pamoja na kuzindua mradi wa maji wa Jimbo(Kidika)
Mhe. Mahundi amewasisitizia Watendaji wa Sekta ya Maji Wilayani Mafia kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na Salama na yenye kutosheleza. Pia, ametoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kwenye Wilaya hiyo kuwa miradi anayetekeleza iweze kukamilika kwa wakati na iendane na ubora wake
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mheshimiwa Zephania Sumaye ameishukru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilayani Mafia ikiwemo miradi ya maji ya Chunguruma-Ndagoni, Kilindoni, kanga, Kibada pamoja na mradi wa maji wa Jibondo.
Post A Comment: