Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda amezindua ligi maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA kwa ajili ya mashindano ya Mchezo wa mpira wa miguu katika Wilaya ya Shinyanga mjini.

Uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa zimamoto (fire) Nguzonane mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM wakiwemo wapunge pamoja na madiwani katika Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe. Mary Chatanda ameipongeza taasisi ya Bega kwa Bega kwa ubunifu huo, kushirikiana na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Shinyanga mjini katika kuandaa mashindano ya mpira ambayo yatatoa fursa za ajira kwa vijana watakao shirikia ligi hiyo.

Mhe. Mary Chatanda akiwa kwenye hafla ya kuzindua ligi ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na jezi zitakazotumiwa na timu 32 ambazo zinashiriki mchuano huo ambao utafanyika kwa zaidi ya Mwezi mmoja.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Bega kwa Bega Mhe. Zainabu Shomar  amesema mashindano hayo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha suala la michezo.

Mhe. Zainabu Shomar ambaye pia ni makamu Mwenyekiti UWT Taifa amesema kuwa  baada ya mchuano huo mshindi wa kwanza atachukua kombe na fedha Shilingi Milioni tano, mshindi wa pili atachukua Shilingi Milioni tatu, na mshindi wa tatu atachukua zawadi ya Shilingi Milioni mbili.

“Tumeandaa mashindano hayo lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassani na tunatarajia kukabidhi kombe na Milioni tano kwa mshindi wa kwanza lakini mshindi wa pili tutampa Milioni tatu na mshindi wa tatu tutampa Milioni mpili”.

“Kwa sasa maadalizi yamekamilika kwa asilimia mia moja, vifaa vipo kila timu itakuwa na jezi zake pamoja na mipira yake tumaamini hakuna changamoto itakayojitokeza”.amesema Mwenyekiti wa Bega kwa Bega Zainabu Shomar

 Mratibu wa mashindano ya DKT. SAMIA CUP SHINYANGA,  Jackline Isaro amemshukuru Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda kwa kuzindua mashindano hayo.

Amesema mashindano DR. SAMIA CUP SHINYANGA  yatatoa fursa mbalimbali kwa vijana na kwamba  timu mbalimbali zikiwemo timu za taasisi za serikali na taasisi binafsi katika Wilaya ya Shinyanga  mjini ikiwemo  timu ya SHUWASA, timu za Bodaboda, timu za Masoko pamoja na timu za Walimu.

Timu zilizopokea vifaa vya michezo kwa niamba ya timu zingine, ni timu ya mpira ya chuo cha St. Joseph, timu ya Ngokolo sekondari pamoja na timu ya Walimu.

Viwanja 8 vitakavyotumika katika mashindano hayo ni uwanja wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga, uwanja wa chuo cha ualimu Shinyanga (SHYCOM), uwanja wa kata ya Old Shinyanga, uwanja wa shule ya msingi Kitangili, uwanja wa kata ya Ibadakuli, uwanja wa Jasko kata ya Ngokolo, uwanja wa Ndala shule ya msingi pamoja na uwanja wa Joshoni kata ya Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Jonathan Madete amewaomba wakazi wa Wilaya ya Shinyanga mjini kujitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo ambapo  kauli mbiu inasema SAMIA VIWANJANI.

  

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Taifa Mhe. Mary Pius Chatanda akiwa katika zoezi la kuzindua ligi maalum ya DR. SAMIA CUP SHINYANGA iliyoandaliwa na taasisi ya Bega kwa Bega kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Shinyanga mjini.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: