Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kasi ya usimamizi wa miradi ya maendeleo katika Mkoa huo itaendelea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 2,2023 wakati akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, baada ya kukamilisha mbio zake  katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga.

Rc Mndeme amesema miradi 41 yenye thamani shilingi bilioni 14.27 imeonwa, kuwekewa mawe ya msingi, kufunguliwa na kuzinduliwa  katika Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Mwenge wa uhuru umekimbizwa umbali wa kilomita 571.5 huku akiahidi kufuatilia na kuisimamia vyema miradi hiyo ikiwemo miradi ambayo imewekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mwaka huu ili iweze kukamilika kwa wakati.

“Kwa niamba na uongozi wa Mkoa na wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuahidi kuwa miradi yote iliyowekewa mawe ya msingi wakati wa Mwenge wa uhuru itafanyiwa ufuatiliaji na usimamizi wa kutosha ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora huku ikisingatia thamani ya fedha”.

 “Kwa miradi iliyozinduliwa na kufunguliwa tutahakikisha kuwa inaendelea kutunzwa vizuri na kutumika kuleta tija na malengo yaliyokusudiwa  kwa maendeleo ya umma kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga aidha kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru nakuhakikishia kuwa maelekezo yote uliyoyatoa kwenye miradi nitayasimamia kikamilifu ili kuona utekelezaji wake unakuwa wa tija kwani katika Mkoa wa Shinyanga chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hakuna kilichosimama”.amesema RC Mndeme

RC Mndeme amesema miradi 11 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 imewekewa mawe ya msingi, miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 imezinduliwa, miradi 4 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 imefunguliwa huku miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni bilioni 1.5 imeonwa na Mwenge wa uhuru 2023.

Ameongeza kuwa jumla ya miti 450000 imepandwa katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga pamoja na kufanyika kwa  huduma ya upimaji wa VVU, Ukimwi, Malaria, uchangiaji wa Damu salama pamoja na elimu kuhusu athari za madawa ya kulevya.

Akizungumza kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Taifa Bwana Abdalla Shaim Kaim amesema kuwa ameridhishwa na hatua za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwapongeza viongozi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.

Mwenge wa uhuru ulipokelewa Mkoani Shinyanga Julai 27,2023 katika Wilaya ya Kishapu na kisha kukimbizwa katika Halmashauri zote sita za Mkoa wa huo ambapo baada ya kukamilika kwa  mbio hizo Mkoa wa Shinyanga umepata hati safi (Clean Sheet).

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema  katika Halmashauri sita za Mkoa huo, Mwenge wa uhuru utakibizwa ubali wa kilomita 755.54 na kupita kwenye jumla ya miradi 59 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 29.

Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2023 unaendelea kukimbizwa katika mikoa mbalimbali Nchini ukiongozwa na Bwana Abdalla Shaim Kaim pamoja na kaulimbiu inayosema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.

Mwenge wa uhuru kitaifa ulizinduliwa April mosi 2023 na kwamba mpaka sasa umekimbizwa katika mikoa 20 ambapo Mkoa wa Geita ni Mkoa wa 21.

Mwenge wa uhuru ukikimbizwa baada ya  kuwasili Mkoani Geita kwa ajili ya makabidhiano leo Jumatano Agosti 2,2023.

Mkimbiza mwenge wa uhuru 2023 akiwa kwenye picha ya pamoja.

Burudani ikiendelea katika eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Nyang’holongo wilaya ya Nyang’hwale mpakani mwa na  Geita.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: