Na
Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wakazi wa kata ya Ngokolo
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wamewaomba Watu wenye mashimo yaliyo wazi
yakiwemo ya maji taka,na vyoo vilivyojaa kuyafukia, ili kuepusha ajali
zinazoweza kusababisha vifo na majeruhi hasa kwa watoto
Kwa nyakati tofauti wakazi
wa mitaa ya Mwinamila,Magadula, Ngokolo Mitumbani na Mapinduzi, wamezungumza kufuatia
uwepo wa mashimo mengi yaliyoachwa wazi ambayo yameonekana kuhatarosha usalama
wa Watu hasa watoto wadogo
Wameeleza kuwa uwepo wa
mashimoyaliyoachwa wazi ni hatari kwa usalama wa Watu,lakini pia yanaweza kuwa
mazalia ya Mbu na wakati mwingine kusababisha mlipuko wa magonjwa hasa wakati
wa msimu wa Mvua
Wameomba viongozi wa serikali
za Mitaa kwa kushirikiana na Maafisa Afya wa kata kuendelea kutoa elimu juu ya
athari zinazoweza kusababishwa na mashimo yaliyoachwa wazi
Akizungumza kwa niamba ya
Mwenyekiti wa mtaa wa Magadula, Mjumbe wa mtaa huo Bi. Winfrida Leonard
amewaomba wakazi wa mtaa huo kuchukua tahadhari kabla ya ajali kwa kufukia
mashimo na kufunika makaro ya maji taka ambayo yako wazi ili kuepusha
athari zinazoweza kuzuilika
Post A Comment: