UMOJA wa matawi ya wanachama , mashabiki na wapenzi
kindaki ndaki wa Klabu ya Simba SC jiji la Tanga wameshiriki kikamilifu
kwenye maadhimisho ya siku ya timu yao kwa kuchangia damu salama
katika Zahanati ya Kisosora ili kuokoa masiaha ya wagojwa wahitaji wa
damu wakiwemo waluopata ajali, wamama wajawazito na watoto waliopo
katika hospital mbalimbali mkoani Tanga .
Akizindua
zoezi hilo Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Japhet Simeo amewapongeza
mashabiki , wapenzi na wanachama wa timu hiyo kwa utayari wao wa kuona
umuhimu wa kuchangia damu ambayo inakwenda kusaidia watu mbalimbali
wenye uhitaji akizitaka taasisi, vikundi na watu binafsi kuendelea kuwa
na utamaduni huo ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofika hospital
kupata huduma hiyo.
"Hongereni
na nawapongeza na nmefurahi sana kwa mashabiki wa timu ya Simba SC kwa
utayari wenu wa kuja kuchangia damu tena kwa hiari yenu, mimi nawaambia
hii ni sadaka na thawabu kubwa sana mliyoitoa kwa wenzenu wenye uhitaji
wa damu , bado uhitaji wa damu katika hospital zetu ni mkubwa kwa sasa
ukilinganisha na wagonjwa ambao wanafika hospitali, hivyo huu uwe ni
mfano wa kuigwa kwa jamii, wananchi .
, taasisi na hata mtu binafsi." alisema Simeo.
Mwenyekiti
wa matawi ya klabu ya Simba SC Edga Mdime alisema kama ilivyo ada yao
ya kila mwaka bado wanasukumwa kuchangia damu katika hospitali
wakitambua kuwa uhitaji wa damu ni mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji
kuongezewa damu hivyo licha ya kushiriki siku hiyo adhimu kwao bado
wanaendelea kuhamasishana kujitoa kwa pamoja katika zoezi hilo.
"Tulianza
na zoezi la usafi lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kuchangia damu na ni
hamasa kubwa sana ambayo imetokea kwa mkoa wetu wa Tanga kwa wanasimba
na matawi yote tumeungana kwa pamoja kwaajili ya zoezi hili la
kuchangia damu"
"Tunajua
damu ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu, damu haihusiani na mwana Simba
, mwana Yanga au yeyote ila damu ni muhimu sana kwa kila mtu haswa
ukizingatia wapo wakina mama wanaojifungua katika hospitali zetu lakini
kuna ajali zinatokea watu wanahitaji kuwekewa damu kwahiyo sisi
tunahamasika kama wanajamii ukiachana na swala la michezo" alisema
Mdime.
Alisema msimu huu
ni wao na lazima makombe yahamie kwao wakijitamba na kikosi kipana
ambacho wanacho msimu huu kulingana na usajili mkubwa uliofanyika
wakiamini lazima timu hiyo ifanye makubwa katika mashindano ya ndani
na hata kimataifa pia.
Mndime
ametuma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za
Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa
kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.
"Niwaambie
kabisa msimu huu tupo tayari kabisa kunyanyua makwapa hapa hapa Tanga
tunaanza na Ngao ya jamii hiyo lazima tuichukue kwa usajili ambao
tumeufanya hatuna shaka na kikosi chetu msimu huu tupo vizuri sana sana
kwa sababu kila nafasi ina mchezaji zaidi ya mmoja tutamfunga Singida na
kwenye fainali yeyote atakayetokea mbele yetu awe Azam au mtani Yanga
lazima tutamchapa" alisema Mdime.
Katika
dimba la CCM Mkwakwani kuanzia Augost 9 Yanga ambao ni mabingwa
watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC
huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya
nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024
kwa kuitwaa ngao hiyo.
Mwenyekiti wa matawi ya timu ya Simba SC Edga Mndime akipata vipimo kabla ya kwenda kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Japhet Simeo(mwenye koti ) akipewa maelezo na mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba baada ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu kwenye Zahanati ya Kisosora
Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba SC wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwenye zahanat ya Kisosora
Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba SC wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwenye zahanat ya Kisosora
Post A Comment: