Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameongea na wanahabari Mkoa wa Mbeya utekelezaji wa ilani ya UWT na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo ametumia zaidi ya shilingi 200m kutekeleza miradi mbalimbali ya wanawake katika Wilaya zote za Mkoa.
Baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika Wilaya zote ni pamoja na ujenzi wa nyumba za biashara pamoja na kalasha lengo ni kuwakwamua wanawake kiuchumi.
Sambamba na hayo kupitia Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) anatarajia kujenga mabweni ya wasichana na kuwalipia mahitaji ya msingi.
Mwisho amewaasa wanawake kuungana ili kuhakikisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao.
Matarajio ni kuandaa tamasha la Mama ntilie(Mama Ntilie Festival 2023) katika wilaya zote za Mkoa wa Mbeya na atatoa majiko 100 ya gesi iwe chachu ya kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Post A Comment: