Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maji Katika Wilaya ya Bagamoyo inayotekelezwa na DAWASA kwenye Mkoa wa Kihuduma Chalinze.
Mhe. Mahundi amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 44.4 na utaboresha huduma ya maji kwenye Wilaya ya Bagamoyo pamoja maeneo ya pembezoni. Pia amewasisitizia DAWASA kuendelea kuwaunganishia wananchi huduma ya maji kwenye majumbani mwao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halma Okashi ameipongeza Wizara ya Maji kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi ya maji na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na pia kuhakikisha inatumika kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Kwa upande Mhandisi Shabaani Mkwanywe amesema mradi huu umejuisha shughuli za Ukarabati na upanuzi wa Mtambo wa maji Wami, Ujenzi wa matanki ya chini na juu 18, ujenzi wa bomba kuu la usafirishaji maji kilimeta 6.258, ujenzi wa mtandao wa usambazaji wenye urefu wa kilimeta 201 na ujenzi wa vibanda vya kuchotea maji 351 kwa Vijiji 59 ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 98.
Post A Comment: