Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa taarifa ya utekelezelezaji wa ilani ya uchaguzi  ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya mwaka 2020/2025 katika kikao mbele ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Dkt Stephen Mwakajumilo katika ukumbi wa shule ya sekondari Mbeya chenye lengo la kupokea utekelelezaji wake.

Akitoa taarifa mbele ya kikao Mahundi amesema tangu achaguliwe kuwaongoza wanawake wa Mkoa wa Mbeya kiu yake ya kwanza ni kujenga mshikamano na umoja na ndani ya jumuia ya Wanawake sambamba na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji kila Wilaya.

Katika hatua nyingine Mhandisi Maryprisca Mahundi amewawezesha wanawake majiko ya gesi zaidi ya mia nane lengo ni kupambana na ukataji wa miti hovyo sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais.

Aidha Mahundi amesema kwa kushirikiana na wanawake atahamasisha wanawake kuhakikisha  wanaunga mkono jitihada za Rais ambapo amebuni kitenge ambacho kimewafikia wanawake zaidi ya elfu moja mia tano kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni hamsini ambacho anakigawa bure.

Hivi sasa Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya zinawezeshwa shilingi milioni ishirini kila Wilaya ili kujiimarisha kiuchumi kwa kujenga vitega uchumi na awali wanawake waliwezeshwa mitaji na sasa tarajio ni kuwawezesha mama lishe katika tamasha maalum litakalojulikana kama “Mama Ntilie Festival”ambapo watanufaika kwa kupatiwa mitaji na majiko ya gesi



Share To:

Post A Comment: