Mapuli Kitina Misalaba ni Mkurugenzi wa MISALABA MEDIA lakini pia ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Radio Faraja FM ya Mkoa wa Shinyanga.

Amezaliwa terehe 28.2.1999 katika kijiji cha Chamva kata ya Idahina Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, ni kijana mwenye hofu ya Mungu ukifuatilia sana ni mtu ambaye anafanikiwa kwa kupitia changamoto nyingi.

 Ni kijana ambaye anapenda sana kufanyakazi yaani mimi huwa namwita kilaka kwa sababu majukumu anayoyafanya utagundua kabisa anauwezo na juhudi za kipekee ambapo ni watu wachache sana wanaoweza kufanya mambo anayoyafanya.

 Ukifika Radio Faraja FM anafanya kazi kila siku hana siku ya kupumzika kama tulivyo wazoea watu wengine yaani kiufupi hana muda wa kupumzika hata kama hayupo kwenye ratiba hawezi kukaa nyumbani.

Hata ukifuatilia historia yake tangu akiwa shule alikuwa anasoma huku anafanya mambo mengi alikuwa mchezaji wa msanii wa Nyimbo za Asili za Kisukuma huku nyumbani walimtegea kwenye kazi za nyumba baada ya kufika sekondari aliokoka akaingia kwenye kwaya kwahiyo alikuwa anatoka shuleni anaenda kwenye mazoezi ya kwaya kanisani lakini mwisho wa siku alifaulu.

Yupo kwenye kitengo cha habari Radio Faraja FM na anamchango mkubwa sana kuanzia Jumatatu hadi Jumapili anatekeleza majukumu yake pamoja na majukumu haya pia yupo kwenye ratiba ya kukesha vipindi vya usiku pamoja na shifti mbalimbali za kusimamia vipindi hapo Radio Faraja.

Kwahiyo anafanya vitu vyote kwenye Online Media yake inayoitwa Misalaba Media bila kuathiri majukumu yake kwenye Radio Faraja.

lakini haishii hapo tu anafanya kazi na Media zingine ikiwemo Matukio Daima, Idawa Media pamoja na Arusha Press Club hebu jiulize ni mtu wa namna gani huyu ndiyo maana mimi huwa namwita kilaka  kwa sababu hata kwenye habari anafanya kazi na watu mbalimbali.

Mimi kila siku nasoma habari zake anazoweka kwenye Misalaba Media uzuri wake anaweza kuandika habari za aina zote yaani za matukio ya Ukatili, maafa, Siasa, uchumi, habari za kijamii ndiyo nyingi lakini pia anaandika mpaka habari za sherehe mbalimbali yaani Mungu aendelee kumbariki sana hata kwenye YouTube kila siku anaposti.

Mapuli Kitina Misalaba pamoja na kuendelea na kazi yake ya uandishi wa habari na utangazaji pia anaendeleza kipaji chake cha mziki ambapo anaimba nyimbo za bongo fleva akitumia jina la Map Master MKM.

Pengine huyu kijana amekosa mtu wa kumshika mkono anaweza kufanya makubwa zaidi ya haya anayoendelea kuyafanya.

Mara nyingi naona namba yake ameiweka kwenye mitandao yake ya kijamii hata wewe unaweza kuwasiliana naye ili uone unamsaidiaje ili aweze kufikia malengo yake katika kuiokoa jamii ya kitanzania, namba yake ni hii 0745594231


Share To:

Misalaba

Post A Comment: