Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa (Mkoa wa Njombe) imeshika nafasi ya ya kwanza Kitaifa kwa mwaka 2023 katika maonyesho ya nanenane kupitia kundi la Halmashauri. 

Wilaya ya Ludewa imetunukiwa Tuzo na Cheti cha Pongezi. 

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa upande wa Ufugaji wa Samaki imeshika nafasi Pili Kitaifa ambapo mfugaji Longinus Mgani kutoka Kata ya Lugarawa Tarafa ya Liganga Wilaya ya Ludewa ameshindanishwa na wafugaji wa Halmashauri zingine na kushika nafasi hiyo ya pili na kushinda tuzo ya pesa taslimu Milioni 6 Tshs na cheti cha Pongezi. 

Maonyesho kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amehitimisha maonesho hayo Mkoani Mbeya Agosti 8-2023. 

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mhe. Sunday Deogratias- Sambamba na wataalam na watumishi wote wa Sekta ya Kilimo Wilayani Ludewa wanawashukuru sana nyote kwa kutembelea Banda la Wilaya ya Ludewa na tunawakaribisha sana kuwekeza katika Kilimo Wilayani Ludewa. 

Share To:

Post A Comment: