Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally.
Na Khadija Kalili
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally amesema kuwa atahakikisha wakulima Wilayani humo wanalipwa malipo yao ya mauzo ya zao la ufuta kwa kukibana Chama Kikuu Cha Ushirika wa Wakulima Mkoa wa Pwani (CORECU) baada ya
Katibu wa Chama Cha msingi cha Wakulima Cha Kisegese Cosmas Ndibia kutuhumiwa kuiba fedha za malipo ya wakulima zaidi ya shilingi millioni 290 za mauzo ya zao la ufuta msimu huu wa 2023/2024.
DC huyo wa Mkuranga Nasri amesema hayo wakati akizungumza na kwa njia ya simu amesema Jeshi la Polisi linamshikilia Katibu huyo wa Chama Cha msingi cha Ushirika wa Wakulima Kisegese kwa uchunguzi zaidi huko Mkuranga Mkoani Pwani.
Amesema kuwa kitu cha kwanza baada ya kumpata mtuhumiwa wa wizi wa fedha hizo ni kukaa na CORECU kuangalia jinsi wakulima watakavyopata stahiki zao kupitia Chama hiko huku hatua za kisheria zitqchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa wizi huo.
"CORECU Sasa watakaa na mtuhumiwa kwa sababu yule ni Kiongozi wao kuangalia ile hela imekwenda wapi na itarudi vipi maana yule ni mtu wao lakini jambo la kwanza ni kuona wale wanaodai waweze kupata haki yao kwahiyo Jmamosi iliyopita tulikaa nao kikao cha mwisho kupitia Afisa Tarafa wa Mkamba hivyo sasa hivi tuna takwimu ya madeni yaliyozalishwa kutokana na ubadhirifu huo uliojitokeza" amesema DC Khadija.
"Sasa tuna kikao Jumamosi na viongozi wa CORECU ngazi ya Mkoa na ngazi ya Wilaya kuweza kuona ni kwa namna gani na hapo tutatoa tamko la namna gani fedha hiyo zitapatikana ili wakulima walipwe fedha zao"
Amesema kuwa kinachofanyika kwa sasa ni kufuatilia ili kubaini ni nani na anadai kiasi gani na alipeleka kiasi cha ufuta ghala kuu la kijiji cha Kisegese ambapo ambapo mwenye taarifa hizo ni huyo Katibu wa Chama hicho Cha msingi kupitia mauzo ya ufuta ya minada iliyofanyika.
Mheshimiwa Khadija amesema kiasi hicho ni cha jumla kuna mkulima mmoja hajapata malipo yao ya ufuta kuanzia kwenye mnada wa nne hadi mnada wa saba wa ufuta.
Amesema kuna wakulima zaidi ya 74 Wilayani humo ambao hawajalipwa kutokana na akaunti zao kuwa na hitilafu mbalimbali na kusababisha fedha kurudi lakini tayari 48 wameshughukia akaunti zao na wameshalipwa malipo yao baada ya kuhakiki akaunti kupitia benki zao.
"Tumekuta kuna mkulima akaunti yake hajaifanyia miamala mwaka mzima akaunti ikafungwa, juna waliokosea namba za akaunti zao ambao tuliwarekebishia pia na ambao fedha zao zinadaiwa kuchukuliwa na Katibu"amesema.
Aidha ametoa ushauri kwa Chama kikuu hicho cha Ushirika wa wakulima Mkoa wa Pwani kuajiri watumishi kutoka miongoni mwa wakulima ambao watakuwa na uchungu na fedha za wakulima.
Post A Comment: