Katibu Mkuu Wizara  ya Maliasili  na  Utalii  Dkt.Hassan Abbas ameitaja   Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori  Tanzania ( TAWIRI ) kuwa ya kimkakati na  umuhimu mkubwa katika sekta ya Maliasili  na utalii  ambapo tafiti za TAWIRI  ni dira   katika kuimarisha  uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Akizungumza na wajumbe wa timu ya menejimenti wakati wa ziara  katika taasisi  hiyo , Dkt. Abbas amesema kipaumbele cha  Wizara ya  Maliasili na Utalii  ni  kuendelea  kuhifadhi maliasili iliyopo  kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Aidha, Dkt. Abbas ameeleza  TAWIRI  ni daraja muhimu  kwa ustawi wa taasisi nyingine za  uhifadhi kwa kutoa ushauri wa kitaalum kuhusiana na wanyamapori " sekta ya uhifadhi inaitegemea  TAWIRI  kutoa mbinu bora zitakazo wezesha uhifadhi na ustawi wa wanyamapori na makazi yao"ameeleza Dkt.Abbas

Dkt. Abbas ametoa wito kwa  Viongozi wa TAWIRI kuhakikisha  umma unapata matokeo ya Tafiti za wanyamapori  zinazofanyika  ili kuzitumia kwa maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Ernest Mjingo  amemshukuru Katibu Mkuu kwa ziara na nakuahidi kupokea maelekezo yote kwa ajili ya utekelezaji.

Share To:

Post A Comment: