Takribani
watu 210 wamejitokeza kupima homa ya Ini katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
ambapo 13 kati yao wameanzishiwa matibabu baada ya kubainika kuwa na
maambukizi.
Watu
hao wamepata huduma hiyo kupitia kampeni maalumu ya kupima na kupata chanjo ya
homa ya Ini iliyotolewa katika Hospitali hiyo, tangu Julai 26 hadi Julai 28
Mwaka huu 2023, ambapo watu 197 hawakukutwa na maambukizi lakini wameshauriwa
juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtaalam wa idara ya magonjwa ya ndani wa
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,Dkt. Emmanuel Sadiki amesema tayari wagonjwa
76 kati ya 197 ambao hawakukutwa na maambukizi, wamepata chanjo ya kujikinga na
homa ya ini, kati yao wanawake ni 42 na
32 ni wanaume.
Dkt.
Sadiki amezitaja baadhi ya dalili za ugonjwa wa homa ya Ini lakini pia madhara
ambapo amesema husababisha kiwango kikubwa cha sumu inayochangia kuharibu mfumo
wa ubongo.
“dalili za awali ni pamoja na kusikia
uchovu,homa,maumivu ya kichwakchefu chefu na wakati mwingine kutapika,lakini
tatizo likikomaa utaona dalili za manjano,maumivu ya tumbo juu upande wa kulia
na dalili nyingine”kwa hiyo ukiona dalili hizo wahi hospitali ili uweze kupata
huduma ikiwemo vipimo,alisema Dkt Sadiki
Hospitali
ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imetoa huduma ya kupima na kutoa chanjo ya homa
ya Ini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya homa ya Ini Duniani, ambapo
zoezi hilo lilifanyika sanjari na utolewaji wa elimu, ushauri na kutoa matibabu kwa watu wanaobainika kuwa na
maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
Dkt.
Emmanuel Sadiki ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa na utamaduni
wa kupima homa ya Ini na magonjwa mengine ili wakibainika kuwa na maambukizi
waanze matibabu mara moja na kwa wale ambao hawatakutwa na maambukizi waweze
kuchukua tahadhari ya kujikinga
Kwa
upande wao wananchi waliopata huduma ya kupima wameshukuru na kupongeza juhudi
za serikali kupitia Wizara ya Afya kuweka utaratibu huo mzuri wa Wananchi kupata
elimu sahihi juu ya huduma za afya,ushauri,kupima chanjo, na matibabu kwa wale
wanaobainika kuwa na maambukizi.
Seleli
Ngassa mkazi wa kijiji cha Jomu kata ya Tinde Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga,ni mmoja wa Wananchi waliopata chanjo ya kujikinga na maambukizi ya
homa ya ini katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shiyanga, baada ya kupimwa na
kukutwa hana maambukizi,ambapo ameeleza kutokana na kupata ushauri na elimu
sahihi juu ya huduma hiyo,amechukua hatua ya kupata chanjo hiyo ikiwa ni tahadhari ya kuzuia maambukizi ya
ugonjwa huo wa homa ya ini
“baada ya kupima majibu yalionyesha
sina maambukizi,kwanza nilifurahi sana,nilitoa machozi ya furaha,na nikamwambia
mtoa huduma anipatie chanjo,kwa kuwa kabla ya kupima,tayari nilikuwa nimepata
ushauri na elimu,kwa hiyo nikapata chanjo hiyo ili kujikinga na maambukizi” ameeleza Ngassa.
Kulthum Mwangia Mkazi wa kata ya Ndala katika
Manispaa ya Shinyanga alisema maboresho yanayoendelea kufanywa na Wizara ya
Afya katika utoaji wa huduma yanasaidia kuzuia vifo vinavyoweza kuepukika.
“inasadia sana kuzuia vifo kwa watu
ambao pengine wasingepata huduma ya kupima wasingebaini tatizo,hali ambayo
ingechangia tatizo kukomaa mwilini na mwisho wa siku hata akifika hospitali kwa
ajili ya kupata tiba,atapoteza maisha kwa kuwa atakuwa amechelewa na tatizo
litakuwa kubwa”amesema Zuhura
MWISHO
Post A Comment: