Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania | SMAUJATA | Wilaya ya Ikungi, Hussein Mseule.
......................................................................

Na Dotto Mwaibale, Ikungi

KAMATI ya maandalizi ya kongamano kubwa na la kihistoria linaloandaliwa na Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania | SMAUJATA | Mkoa wa Singida inatarajia kufanya ziara ya siku moja wilayani Ikungi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Smaujata Wilaya ya Ikungi, Hussein Mseule alisema ziara hiyo ambayo itafanyika kesho Agosti 29, 2023 kwao ni ya muhimu kwa kuwa itawahusisha viongozi mbalimbali wa Smaujata ngazi ya mkoa wakiongonzwa na Mwenyekiti wao Dismas Kombe.

‘’ Ziara hii kwetu ni ya muhimu na itakuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi mbalimbali kutoka mkoani kufika hapa kwetu kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kubwa likiwa ni maandalizi ya kongamano letu litakalofanyika Oktoba 7, 2023.

Alisema viongozi hao watafika saa moja kamili kesho asubuhi ambapo watatembelea ofisi ya mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, ofisi ya Ustawi wa Jamii na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii na baada ya hapo kitafanyika kikao ambacho pamoja na mambo mengine kitahusu kongamano hilo na kuhamasisha makundi mbalimbali kuchangia fedha za maandalizi.

Mseule alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi na Mashujaa wote wa Smaujata wilayani humo kujitokeza kwa wingi kufika kwenye kikao hicho kwa lengo la kufanikisha maandalizi ya kongamano hilo.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Dismas Kombe aliwaomba viongozi wote wa Smaujata kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata, wilaya hadi mkoa kuendelea kujitoa usiku na mchana kuhamasisha wanasmaujata na makundi mengine kuwaunga mkono kuchangia maandalizi ya kongamano hilo.

Kombe alisema kwa mtu yeyote, Taasisi, Wafanyabiashara, makundi mengine na madhehebu ya dini watakao wiwa kuwaunga mkono kwa kuwachangia ili kufanikisha kongamano hilo wanaweza kuwasiliana na waratibu wa kongamano hilo, Dismas Kombe kwa namba ya simu 0758489886,, Makamu Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Singida, Ambwene Kajula kwa namba ya simu 0713343687 na Mwenyekiti wa kongamano hilo, Juma Amrani kwa namba ya simu   00763850879 na kuwa kutoa ni moyo na sio utajiri.

Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo ni Omari Mwangi Makamu Mwenyekiti, Mwenyekiti Juma Amrani, Katibu, Beatrice Claudi na Mweka Hazina Elineema Babu.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: