NA DENIS CHAMBI, TANGA.
HALMASHAURI ya jiji la Tanga imeongeza ukusanyaji wake wa mapato ndani kupitia vyanzo vyake ikikusanya kutoka shilingi billion 15 hadi shilingi Billion 18.2 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akizungumza katika kikao cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 mstahiki meya wa halmashauri ya jiji la Tanga Abdurahman Shillow amesema kuwa katika billion 18.2 tayari wameshakusanya billion 17.8 na hiyo ni kutokana na ushirikiano uliopo baina ya watumishi sambamba na ziara waliyofanya katika halmashauri ya Chalinze mkoani Bagamoyo ambayo walienda kujifunza nayo imeweza kuzaa matunda.
"Tumetengenezewa halmashauri yetu tumetoka katika mahali pagumu lakini sasa hivi yupo sehemu nzuri, tumetoka kukuanya billion 15 sasa hivi tupo kwenye billion 18.2 na katika hizo tumeshakusanya billion 17.8 na sasa hivi tupo kwenye bajeti ya billion 19" alisema Shillow
Aidha amesema kuwa Halmashauri ya jiji la Tanga ilikuwa hainufaiki na chochote kutokana na uwepo wa madini ikishindwa kukusanya lakini kufwatia ziara waliyoifanya Chalinze mkoani Bagamoyo imewawezeaha sasa wanakusanya billionmpaka 4 kwa siku.
"Lakini mtu asijekusema yeye ndiye alikuwa sababu ya kupanda kwa mapato haya, mapato haya yamepandishwa na watendaji wetu wote wa kila idara ila chini ya usimamizi mzuri na chanzo cha mapato haya ni kutokana na ziara tuliyoifanya Chalinze sisi tulikuwa hatupati hata kitu kwenye madini baada ya ziara ya Chalinze tukaja tukabadilisha sheri yetu ndogo tukajikuta sasa tunapata mpaka billioni mpaka 4 kwa siku." Alisema Shillow.
Akizungumzia kuhusu uwekezaji katika bandari ya Dar es salaam unaofanywa na wawekezaji kutoka Dubai DP World , Shillow alisema kuwa halmashauri inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na serikali katika uboreshaji wa bandari hapa nchini.
"Jiji la Tanga tunatekeleza juhudi zote zinazofanywa na serikali katekeleza ilani ya chama cha mapinduzi hususan katika kipengele cha uwekezaji cha kuimarisha na kuboresha miundombinu ya bandari zetu nchini watu wa Tanga tupo na mheshimiwa Rais tunamwambia akaze buti tusonge mbele watu wa Tanga tuna imani na yeye" alisema Mstahiki meya huyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi 'CCM' wilaya ya Tanga Meja Hamis Mkoba ameitaka halmashauri hiyo kuzifanyia kazi hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' ikiwemo kukamilisha miradi yote viporo ifikapo September 2023 na hatimaye iweze kufanya kazi.
"Miradi viporo ambayo imetajwa kwenye ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali 'CAG' na haikumalizika tunawaagiza watendaji wote ifikapo september iwe imeshakamilika watendaji wote waendelee kuisimamia kulingana na agizo alilolitoa mkuu wa mkoa" alisisitiza Mkoba .
Post A Comment: