Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata vitu mbali mbali vya wizi ikiwemo Mawe yenye madini ya dhahabu uzito wa gram 6753.2 yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.2, katika mgodi wa Bulyankulu Wilayani kahama Mkoani Shinyanga.

Katika taarifa yake leo Jumatano Agosti 23,2023 kwa vyombo vya habari kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,kamishina msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema vitu pamoja na vielelezo hivyo vimekamatwa kufuatia msako mkali uliofanya na askari wa jeshi hilo katika kipindi cha Julai na Augusti Mwaka huu.

Amevitaja vitu vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na mawe yenye madini ya dhahabu,carbon yenye madini yanayodhaniwa kuwa ni dhahabu,Bunduki aina ya raifo,Mafuta aina ya disel ambavyo vilikutwa katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Shinyanga.

“Tumekamata lita 603 za mafuta aina ya Diesel katika maeneo tofauti ya mradi wa Reli ya mwendokasi SGR, pia tumefanikiwa kukamata mawe yenye madini ya Dhahabu yenye uzito wa gramu 6753.4 na thamani ta Shilingi 9,213,116.83/= huko katika mradi wa machimbo ya dhahabu ya Bulyanhulu lakini pia tumekamata Carbon yenye mchanga wenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenye uzito wa Kg 261 ambayo thamani yake bado haijajulikana huko maeneo ya Manzese Kahama.

Aidha katika misako hiyo tumefanikiwa kukamata Bunduki aina ya Riffle yenye namba 2/29pf78701 ambayo ilikuwa inatumika katika shughuli za ulinzi bila kibali, pia tumekamata madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kg 71, seti moja  ya Computer, Pikipiki tatu, Tiles Box 14, mabomba sita ya chuma na vipande tisa, mabati 17, Plastick tatu za rangi ya majumba, vipodozi vinavyoaminika kuwa ni sumu tayari jumla ya watuhumiwa 31 wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi kuhusiana na makossa hayo na wengine wamepewa dhamana huku wakisubiri kufikishwa  Mahakamani”.amesema Kamanda Magomi

Kamanda Magomi amesema katika Msako huo Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 31 wanaosadikiwa kuhusika na wizi wa mali na vielelezo vilivyokamatwa, ambao wanashikiliwa katika vituo mbali mbali Mkoani Shinyanga.

Ameeleza pia kwamba kesi mbalimbali zilizofikishwa mahakamani na jeshi hilo washitakiwa wamepata adhabu mbali mbali ikiwemo hukumu ya vifungo jela, na wengine kulipa faini.

“Kwa upande wa mafanikio Mahakamani jumla ya kesi 34 zilipata mafanikio Mahakamani lakini upande wa usalama barabarani jumla ya makossa 4017 yalikamatwa”.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linapenda kuwaasa wananchi wote kwa ujumla kufuata sheria za Nchi na pia kutoa ushirikiano kwa jeshi ili kudumisha amani na utulivu uliopo”.amesema kamanda Magomi

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga  kamishana msaidizi wa polisi  Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 23,2023.

 Mwonekano wa vitu mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia misako iliyofanyika kuanzia Mwezi Julai hadi Agosti 22 Mwaka huu 2023.

Share To:

Misalaba

Post A Comment: