Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) leo kimetangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi waliotayari kujiunga na Chuo kwa mwaka wa Masomo 2023/2024 katika ngazi ya Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree Programmes) kwa kozi tano. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Kampasi ya Chuo iliyoko Dar es Salaam Prof. Eliamani Sedoyeka, Mkuu wa Chuo amempongeza  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi (Samia Scholarship) kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na amesema, " IAA kama Chuo tunamuunga mkono Mhe. Rais kwa kutoa ufadhili wa masomo katika kozi zetu mpya lakini pia kozi ambazo tunaona ni za kimkakati na zinauhitaji". 

Prof. Sedoyeka amezitaja kozi hizo zinazotarajiwa kutolewa ufadhili kuwa ni:-
1. Shahada ya Ukaguzi wa Hesabu na Uhakikisho (Bachelor Degree in Auditing and Assurance)
2. Shahada ya Media Anuwai na Mawasiliano kwa Umma (Bachelor Degree in Multimedia and Mass Communication)
3. Shahada ya Usimamizi wa Nyaraka na Taarifa (Bachelor Degree in Records and Information Management)
4.  Shahada ya Usimamizi wa Mikopo (Bachelor Degree in Credit Management)
5. Shahada ya Ukutubi na Sayansi ya Taarifa (Bachelor Degree in Library and Information Science)

Aidha, ametoa wito kwa wanafunzi wote wenye nia na hamasa ya kusoma katika Chuo cha Uhasibu Arusha kutumia fursa hii kuomba ufadhili wa kusoma masomo haya, ambapo amesema anaamini  kwamba kupitia uchaguzi wao wa masomo na bidii, wataweza kufikia malengo yao ya kielimu na kuchangia katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Akifafanua utaratibu wa maombi hayo ya ufadhili amesema maombi ni bure na wote wana fursa za kufanya hivyo.

 Ameeleza kuwa taratibu na maelezo ya kupata ufadhili  yanapatikana katika tovuti ya Chuo www.iaa.ac.tz na sifa kubwa uwe na vigezo vya kudahiliwa katika programme husika kulingana na vigezo vilivyoweka na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Share To:

Post A Comment: