Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohamed Ali Kawaida (MCC) amesema ziara anayoifanya katika Mkoa wa Kaskazini Unguja lengo lake ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 na sio kupiga picha. Ameyasema hayo tarehe 11 Agosti, 2023 alipowasili Mkoa wa Kaskazini kuanza ziara yake ya kakazi visiwani Zanzibar.


"Leo tumekuja na kamati ya utekelezaji kwa ajili ya mambo matatu,  moja ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi. Sisi hatujaja kupiga picha bali tumekuja kuwaelezeni ni wapi tulipofikia katika utekelezaji wa Ilani ya CCM na ndio maana tumewataka wawakilishi wa serikali wakiwemo wakuu wa Mikoa,  wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wawepo ili watueleze ni wapi wamefanya na wapi wamekwama katika utekelezaji wa Ilani ya CCM" alisema Komredi Kawaida.

Aidha Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC) amewapongeza vijana wa Mkoa wa Kaskazini kwa kuendelea kufanya Siasa nzuri na za kistaarabu.

 "Niwapongezeni sana vijana wenzangu wa Mkoa wa Kaskazini,  mimi nimekuwa mmoja wa ufuatiliaji wazuri wa siasa za ndani na nje ya Zanzibar,  hakika mmekuwa ni watu wenye siasa nzuri na za kistaarabu hongereni sana.

Katika ziara hiyo Komredi Kawaida ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM-Taifa, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi wanaowakilisha kundi la Vijana na Wabunge wa Vijana.

Share To:

Post A Comment: