NA DENIS HAMBI,  TANGA.

Serikali imesema kuwa  imepokea pendekezo na maombi ya wawekezaji wa ndani na nje walionyesha nia ya kuvihuisha viwanda vilivyokufa ndani ya mkoa wa Tanga  ili kuvirudisha upya ili viendelea kufanya kazi na wanchi waweze kupata maendelo  na hatimaye  kuweza kuchangia  pato la Taifa.

Akizungumza katika kikao cha pamoja na wafanyabiashara wa mkoa wa Tanga waziri wa viwanda na biashara  Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa  tayari wizara ilishatuma timu ya wataalam kwaajili kufanya tathmini ambao tayari wameshamaliza na sasa imebakia kutoa mikataba kwa wawekezaji walioonyesha nia.

"Wizara imeandaa mikataba mipya yenye kupimika kwa vipindi vifupi vifupi tutakutaka ufanye vitu tulivyokubaliana ukishindwa tutaachana na wewe  tunatafuta mwekezaji mwingine afanye kazi kwenye  eneo hilo na wapo wengine mtaona wataanza siku sio nyingi,  timu ya msajili wa hazina ilikuwa Tanga wakishughulikia mambo hayo hayo na sisi kama wizara tulishamaliza kuyaandikia yote".alisema Dkt Kijaji.

"Wenye dhamira ya dhati tutawapa mikataba kwa vipindi vifupi vifupi wakishindwa  basi tutaachana nao tuendelee kupata wawekezaji wengine ili Tanga  irejee kuwa ni mkoa wa viwanda kama ilivyokuwa tangu mwanzo" alisisitiza

Aidha Dkt Kijaji aliyaagiza mabaraza ya biashara kuanzia ngazi ya wilaya kuhakikisha wanatoa taarifa  mapema ili timu za wataalam kutoka wizarani ziweze kushiriki ili kubeba na chukukua changamoto na mapendekezo mbalimbali yatokanayo na hatimaye kwenda kuyafanyia kazi.

"Tumeamua kwenye mabaraza yote ya biashara ya wilaya wizara itakuwepo kwenye mabaraza yote ya biashara ya wilaya zetu zote ndani ya taifa letu,  tunaomba sana tupeane taarifa  ili kwenye vikao hivyo wakurugenzi  na wataalam wetu wawepo na kusiwe na jambo lolote la kuchukua sisi ya kwetu ni kumaliza changamoto zote  ambazo wanazipitia wafanyabiashara"

Alisema bado serikali itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa sekta binafsi zilizopo hapa nchini hususan wafanyabiashara  hivyo katika kuendelea kuzilea imeweka mazingira rafiki na madhubuti za kuhakikisha kuwa zinaendelea kuku na kuleta maendeleo kwa taifa.

"Rais wetu anaamini na ameamua kuwakabidhi uchumi wa Tanzania sekta binafsi ya taifa hili hasa wafanyabiashara,  hakuna taifa lolote ambalo liliwahi kufanikiwa bila kuwa na sekta binafsi ambayo ni imara, shindani ndani ya taifa lakini hata nje ya taifa hilo hivyo Rais anatuambia ataendelea kusimamia misingi itakayowezesha sekta binafsi ya Tanzania ikue  na siku moja tuendeshe Afrika na dunia kutoka Tanzania" alisema Waziri Kijaji.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alisema mkoa umekuwa ukitatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara na bado inaendelea na zaidi ya yote kuwawekea mazingira rafiki wafanyabiashara  ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato na hatimaye waweze kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.

"Tumeendelea kufanya mikutano mbalimbali ya wajasiliamali na majukwaa mbalimbali ya kibiashara  na kupitia mikutano hiyo tukasema Tanga tupo tayari kwaajili ya kufanya biashara hatutakwenda kufunga biashara wala akaunti ya mfanyabiashara yeyote kama ambavyo mheshimiwa Rais amekuwa akituasa mara kwa mara kwamba ni muhimu kutengeneza mazingira rafiki ya wafanyabiashara kwenye mikoa yetu" alisema Kindamba


Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara katibu wa  jumuia ya wafanyabiashara mkoa wa Tanga 'JWT' Ismail Masoud alisema  kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo katika wilaya za Lushoto na Handeni ambao wamepelekwa mahakamani wakishitakiwa na halmashauri zao kwa kushindwa kulipa kodi kulingana na mikataba waliyoingia jambo ambalo ameomba kumalizwa kero hiyo ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo wadogo waweze kujipatia kipato.

"Kumekuwa na shida ya halmashauri zetu sasa hivi za Lushoto na Handeni wafanyabiashara hawa wadogo wadogo wanashtakiana na halmashauri kwa mikataba waliyoingia nayo kwa hiari kabisa ikifika miaka miwili tu wanafuta ule mkataba na wanaanza kuwadai wafanyabiashaa kodi kubwa sasa hivi kuna kesi katika mahakama za wilaya ya lushoto na Handeni

Share To:

Post A Comment: