Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga akizungumza wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni na sanaa Mkoa wa Lindi iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo mkoani humo jana.
............................................
Na Dotto Mwaibale, Lindi
WASANII mkoani Lindi wametakiwa kuchangamkia fedha Sh.Bilioni 20
zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kama ruzuku za kuwawezesha kukopa ili
kuwasaidia kuinua vipato vyao kupitia kazi zao za sanaa.
Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga wakati
akifungua warsha ya kuwajengea uwezo
wadau wa utamaduni na sanaa Mkoa wa Lindi iliyoandaliwa na Wizara ya
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
"Hizi fedha zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili yenu
hivyo changamkieni fursa hiyo kwa kuboreha shughuli zenu ili muweze kujikwamua
kiuchumi," alisema Ndemanga.
Alisema wadau wa Sanaa watakaokidhi vigezo vilivyoweka ndio watakaokopeshwa
fedha hizo kupitia mfuko ulioanzishwa na Rais Samia ambapo aliwahimiza wasanii
hao kuhakikisha wanakithi vigezo hivyo ili waweze kukopesheka na kuwa fedha
hizo sio zawadi bali zinatakiwa kurejeshwa ili ziweze kukopeshwa kwa wengine.
Shahibu aliwataka wasanii hao na wadau wa utamaduni kujiendeleza kielimu
ili kwenda na dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia huku wakianzisha miradi
mbalimbali kama ufugaji,kilimo, na mingine badala ya kutegemea sanaa peke yake.
Aidha, aliwataka wasanii hao kujenga
tabia ya kushirikiana na taasisi zingine wakati wa kufanya shughuli zao jambo
ambalo litawaongezea uzoefu wa masuala mengine ya maendele na sanaa kwa ujumla.
Alisema Serikali inatambua mchango wa wasanii na kuwa kwa siku za hivi
karibuni imeonekana kazi nyingi za wasanii kama filamu na tamthilia zikioneshwa
zaidi na vyombo vya habari vya watu binafsi hivyo watawasiliana na wahusika wa
vyombo vya Serikali kuona namna ya kuanza kutumia kazi za wasanii hasa
chipukizi katika vyombo hivyo.
"Changamoto kubwa iliyopo ni uzingatiaji wa maadili katika kazi zetu
nawaombeni mkawe mabalozi wazuri wa kusimamia maadili ya kitanzania na si
vinginevyo na kuacha kutengana kwa sababu ya migogoro yakugombea fedha na sisi
kama Serikali hatutakuwa tayari kuona mambo hayo yakitokea," alisema
Ndemanga.
Awali akitoa taarifa ya mfuko huo Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tazania
Nyakaho Mahemba alisema mfuko huo unatoa huduma katika maeneo ya urithi wa
utamaduni , lugha na fasihi, sanaa za maonyesho, ufundi , filamu, muziki na fani
nyingine zenye mlengo wa utamaduni na sanaa kwa watu binafsi,
vikundi au makundi.
Alitaja huduma zinazotolewa na mfuko huo kuwa ni mikopo ya uendeshaji yenye lengo
la kuwezesha shughuli za kiutendaji wa kila siku za uzalishaji wa kazi
za utamaduni au sanaa.
Alitaja kazi nyingine ni utoaji wa mikopo ya vifaa yenye lengo la kuwezesha ununuzi wa vitendea kazi vya uzalishaji za utamaduni au sanaa na
mikopo ya kujikimu/ dharura ambayo ni mikopo ya muda mfupi inayotolewa kwa
lengo la kujikimu wakati wa safari za
kuandaa au kufanikisha kazi za utamaduni
au sanaa.
Alisema lengo la mafunzo ni kuongeza ujuzi na thamani ya kazi za utamaduni na sanaa ili ziwe na
ubora unaoendana na mahitaji ya soko.
Mahemba alisema kulingana na kuingia makubaliano na Benki ya CRDB na Serikali kupitia mfuko huo walengwa wa mfuko watakaohitaji
huduma za mikopo watatakiwa kuwasilisha maombi yao
kwa njia ya posta, barua pepe au
moja kwa moja katika ofisi za
mfuko huo kwa ajili ya mapitio ya awali ya kitaalamu kisha maombi hayo kufikishwa katika Benki ya CRDB
kwa hatua zao.
Msanii wa ngoma za asili Salum Namtitili akizungumza kwa niaba ya wenzake
alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha hizo kwa lengo la
kuwainua kiuchumi.
“Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha wasanii kwani tulikuwa na changamoto kubwa ya kuendeleza sanaa zetu lakini kwa fedha hizi tutasonga mbele kwani tutaweza kutoka sehemo moja kwenda nyingine na kurekodi kazi zetu tofauti na ilivyokuwa zamani tukiangaika kutafuta fedha huku na kule bila ya mafanikio,” alisema Namtitili.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga (katikati) akiwasili Hoteli ya Sea View Hotel and Resort kwa ajili ya kufungua warsha ya kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni na sanaa Mkoa wa Lindi iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tazania Nyakaho Mahemba akitoa taarifa ya mfuko huo.
Afisa Utamaduni Mkoa wa Lindi, Makalaghe Nkinda, akizungumza kwenye warsha hiyo.
Afisa Mwandamizi wa Mkopo wa Benki ya CRDB kutoka Makao Makuu, Alpha Mgubila, akizungumza kuhusu mikopo itakayokopeshwa kwa wasanii kupitia benki hiyo.
Mwenyekiti wa Wasanii Mkoa wa Lindi, Athuman Mohamed akizungumza kwenye warsha hiyo.
Msanii wa ngoma za asili, Salum Namtitili, akitoa shukurani kwa Rais Samia kwa kutoa fedha hizo.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa warsha hiyo.
Wasanii wakiwa kwenye warsha hiyo.
Viongozi wakiimba wimbo wa kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha hizo.
Wasanii wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi |
Post A Comment: