NA DENIS CHAMBI, TANGA.
BENKI
ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa wadau wakiwemo walimu wa
shule za msingi na sekondari ambapo imekuja na huduma ya Mwalimu Spesho
yenye lengo la kuwawezesha na kuwainua kiuchumi ikiwa ni pamoja na
kuwapa fursa za mikopo kwaajili ya biashara, kilimo na ada.
Zaidi
ya walimu 300 kutoka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari
mkoani wa Tanga wameshiriki warsha iliyoandaliwa na Benki hiyo ya NMB
kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuwapa elimu juu ya huduma na fursa
mbalimbali zikiwemo elimu ya kifedha, na elimu ya bima.
Akizindua
Warsha hiyo mkuu wa wilaya Tanga James Kaji ameipongeza Benki hiyo kwa
kundelea kuboresha huduma zake kwa wadau wa hususan wa serikali
akiwataka walimu kutumia fursa za mikopo zinazotolewa kwaajili ya
kuwainua wateja wake hasa kiuchumi, kielimu , kwenye sekta ya kilimo
akiwataka kuachana na mikopo umiza ambayo wamekuwa wakiipata sehemu
nyinginezo.
Aidha Kaji
alisema kwa kuwainua kiuchumi walimu itawasaidia pia kuwawezesha hata
kiutendaji katika majukumu yao ya kiufundishaji hatua ambayo itasaidia
kuwaandaa wanafunzi bora kitaaluma na maadili mema.
"Nitoe
pongezi kubwa sana kwa Benki ya NMB kwa kuandaa kongamano hili kila
mwaka kwa walimu imetoa msisitizo mkubwa na kuwawezesha walimu, wazo la
kuwafikia walimu hususan katika kuwawezeaha kimikopo ni zuri na la
kuigwa , na nyinyi walimu onyesheni jithada na uwezo wenu katika
kuchangamkia na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana"
"Walimu
wengi katika shule zetu za msingi na sekondati wengi wao walikuwa
wakijiingiza katika mikopo umiza ambayo imefanya wanashindwa kutekeleza
majukumu yao ya kila siku lakini kwa fursa hizi zinazotolewa, na
tumeshuhudia wengi wao kutokana na mikopo inayotokana na NMB
wameboresha maisha yao kutokana na huduma jinsi ambavyo wameweza
kuinuka kimapato na kuboresha maisha yao ya kila siku" alisema Kaji.
Awali akizungumza mkuu wa kitengo ya Bima kutoka benki ya NMB kanda ya kaskazini Martin Masawe kwa
niaba ya afisa biashara na wateja binafsi amesema kuwa walimu wana
nafasi kubwa ya kunufaika na huduma mbalimbali wanazozitoa huku wakiwa
na lengo la kuwafikia walimu wote nchi nzima.
"Tumekuwa
tukitoa elimu ya kifedha, elimu ya bima na elimu mbalimbali za
kujipangilia kimaisha kwa walimu, bila mwalimu pengine sisi
tusingekuwepo hapa na umuhimu wa walimu katika benki yetu ni jambo
kubwa na la umuhimu sana tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka na tumepanga
kuwafikia walimu wote nchi nzima na kwa mwaka huu tunategemea kuwafikia
walimu 9000 katika wilaya na mikoa mingi zaidi sambamba na kutoa elimu
kwa walimu wote" alisema Massawe
"Benki
ya NMB iliangalia ni kitu gani cha kipekee ambacho anaweza kupata
mwalimu kutoka kwetu kwahiyo tulitengeneza masuluhisho kulingana na
maisha yao ambapo tunayoa mikopo kwaajili ya elimu pale wanapotaka
kujiendeleza au mtoto wake anaweza kupata mkopo wenye riba nafuu ya
9%, tunatoa mikopo ya kilimo , tunatoa pia mikopo kwaajili ya vyombo
vya usafiri kwaajili ya kujiongezea kipato zaidi ya kile ambacho
anakipata mwalimu" alisema Massawe
Baadhi
ya walimu akiwemo Coletha Joseph na Maurus Ndunguru ambaye ni kaimu
afisa elimu wa halmashauri ya jiji la Tanga wameishukuru na kuipongeza
Benki hiyo kupitia mikopo na huduma ambazo wanazipata zitakazowasaidia
kuwainua kiuchumi na kuwapa fursa ya kujiendeleza kimasomo na katika
maisha ya kawaida.
"Tunaishukuru
sana Benki ya NMB kwa kutuona na kutuletea huduma mbalimbali hasa ya
mikopo ambayo itatusaidia kutuongezea kipato nje ya kazi yetu tutakwenda
kuwaelimisha na wenzetu juu ya fursa hizi zinazopatikana ili waweze
kuzitumia na kusaidia kuongeza kipato kwa ujumla " alisema Coletha.
"Huduma
hizi wanazozitoa benki ya NMB ni nzuri zitaboresha miasha ya walimu
kwasababu tumekuwa tukizunguka sana kwenye mambo ya mikopo ambayo
inaumiza wakati mwingine lakini kwa kuja kwao NMB hapa kutawasaidia sana
walimu" alisema Ndunguru.

Baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka wilaya mbalimbali mkoani Tanga wakiwa wanafwatilia elimu ya fedha inayotolewa na benki ya NMB katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach.
Post A Comment: