Na Moreen Rojas,Dodoma.

Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili Mradi wa utafiti wa kusaidia somo la hisabati  kutokana na matokeo mabaya ya somo hilo katika matokeo ya Darasa la saba na  kidato Cha nne nchini ili kumaliza tatizo hilo.

Akizungumza leo Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt.Amos Nungu amesema kuwa imeidhinisha miradi miwili (2) kwa thamani ya TZS 120M kwa kila mradi.



Dkt.Nungu amesema Miradi mingi ya utafiti hufadhiliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ambao kwa sasa ipo miradi kadha inayoendelea na ipo hatua mbalimbali ambayo Serikali ilifadhili kupitia COSTECH.


"Majukumu ya COSTECH ni kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti, uratibu, kuendeleza na kuhawilisha teknolojia na ubunifu, kukusanya, kuhifadhi na kusambaza taarifa za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na kutafuta fedha kutoka serikalini na wadau wengine kwa ajili ya kukuza na kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu"


"Vilevile ni kukuza mahusiano ya kikanda na kimataifa katika masuala ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, kushauri Serikali kuhusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu yakiwemo vipaumbele vya utafiti, mgao wa matumizi ya fedha za utafiti kufuatana na vipaumbele vilivyokubaliwa, mafunzo na ajira za watafiti na Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia"Amesisitiza Dkt.Nungu


Dkt.Nungu amesema Serikali kupitia COSTECH imeidhinisha jumla ya miradi saba (7) kwa thamani ya TZS 150M kila mradi itakayofanyika ndani ya miaka miwili na kuhusisha watafiti na wabunifu kutoka sekta zote.



"Kuwasaidia DTBi kukamilisha karakana iliyopo SIDO Vingunguti ili kuzalisha mita kwa wingi na kwa wakati kukamilisha ufungaji wa mita hizo za maji kwa mikoa 15 iliyobaki, kusimamia Kongano Bunifu mpya ikiwemo ya Mafia (nazi) na Kigoma (mawese) na kufanya kazi na kumbi za Bunifu na wadau wengine kuhakikisha mazingira wezeshi yanaimalika zaidi"Amesema Dkt.Nungu



Amesema COSTECH inaendelea kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuanzisha au kutoa usaidizi kwa vituo mbalimbali vya ubunifu ili kuwafikia na kuwahuduma wabunifu kiurahisi. Mazingira wezeshi kwa ujumla wake katika ubunifu ni pamoja na kuwa na mfumo stahiki inayosaidia wabunifu na bunifu nchini ,ikiwa ni pamoja na Kumbi za Ubunifu kuwapokea na kuwalea wabunifu, Sera na miongozo Pamoja na mitaji.


Katika kuratibu Utafiti na Ubunifu, COSTECH inaendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali, kubwa ikiwa ni kufanikisha kuweka mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha, sera na miongozo stahiki, mashirikiano, miundombinu, nk. ili kuhakikisha mchango wa utafiti na ubunifu unaleta manufaa kwa taifa.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: