Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suruhu Hassan imeweza kutatua changamoto ya umeme katika Wilaya ya Urambo na Mkoa wa Kigoma ambapo zaidi ya Bilion 30 zimeletwa katika kuhakikisha zinajenga Kituo Cha Kupoza Umeme katika Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Akizungumza katika Ziara ya Wilaya hiyo  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amewapongeza Kampuni ya TBEA_ CHINA na  uongozi wa Tanesco na Serikali kwa ujumla kwa kusimamia kikamilifu mradi huu ambao utakuwa chachu ya kuondoa Changamoto za umeme katika baadhi ya Vitongoji.

Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya awamu ya sita inalengo la kuondoa hadha ya umeme kwa wananchi  wake katika kuhakikisha wanapata umeme kila sehemu na kwasasa niwaombe wananchi kuhakikisha mnalinda Miundombinu ya umeme katika maeneo yenu.

" Nimeona maeneo mengi uwa wanachoma moto nguzo hivyo niwaombe wananchi wangu kuwa makini na kulinda Miundombinu ya Tanesco  katika maeneo yenu ili Serikali hizidi kuleta fedha nyingi na kuepusha umeme kuzimika zimika."

Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amefurahishwa na ajira ya vijana ambao wanafanya katika Ujenzi huo  wanatoka katika Wilaya ya Urambo na Wilaya jirani za Mkoa wa Tabora kwa kuwa sisi kama Viongozi tunahimiza kuwajali na kuthamini wazawa ambao wapo katika eneo la mradi ili wawe chachu ya kuwa walezi wa Mradi huo.

"Mwenyekiti Chatanda amewasii vijana ambao wamepewa ajira hapo  kuwa waaminifu na waadilifu katika kulinda vifaa na Miundombinu iliyopo katika mradi huo ili mradi umalize kwa wakati na uwe bora zaidi ."







Share To:

Post A Comment: