Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda ametembelea Kituo Cha Afya Maili Tano kilichojengwa kwa gharama ya sh Milion 400 katika Wilaya ya Tabora Mjini.
Akizungumza leo katika Ukaguzi wa Kituo hicho Mwenyekiti Chatanda ametatua changamoto ya Maji katika Kituo hicho Cha Afya kwa kumpigia simu Naibu Waziri Marryprica Mahundi ambaye amekiri kuchimba kisima katika Kituo hicho.
Mwenyekiti Chatanda amesema Kituo Cha Afya kama akina Maji wanawake wengi wanapata shida wakati wa kujifungua kwa kuwa wanahitaji Maji mengi ili yawasaidie katika kujifungua hivyo naomba nikupongeze sana Naibu Waziri wa Maji kwa kulitatua changamoto hii.
"Maji ni uhai Maji ni muhimu sana katika taasisi zozote zile za Umma hivyo niwatake Ruwasa muendelee kusambaza Maji katika taasisi za Umma kwa kuwa wananchi wengi wanahitaji huduma ya Maji"
Post A Comment: