Na John Walter-Babati

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Babati Mjini wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Dr. Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza vyema ilani ya Chama kwa Miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Wameyazungumza hayo leo Agosti 26,2023 katika kikao Cha majumuisho ya ziara ya kamati ya siasa Babati Mjini na watumishi wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama.

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM) Babati Mjini Elizabeth Marley, amesema awamu nyingi za Marais wa Tanzania zimepita lakini hii ni funga kazi kwani kila kata mafundi wapo bize kujenga na kukarabati Miradi ya Afya,elimu,Maji na barabara.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema serikali itaendelea kusimamia huduma zote za kijamii ili ziwafikie Wananchi kwa ubora unaotakiwa.

Amesema serikali imeshatoa pesa nyingi kwa ajili ya miradi hiyo na wao watahakikisha kila shilingi inatumika kama ilivyokusudiwa na atakaekwenda kinyume atawajibishwa.


Share To:

Post A Comment: