Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imewanoa waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha na kuwajengea uwezo wa kutafuta na kuripoti kwa usahihi taarifa za ukaguzi na udhibiti wa fedha za umma ikiwemo sheria,kuichambua ripoti na misingi ya mawasiliano baina ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Vyama vya Waandishi wa Habari,
Waandishi hao wa habari wamejengewa uelewa juu ya mbinu za kutambua aina za ripoti za ukaguzi, Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mwakilishi wa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mkaguzi Mkuu wa Nje (CEA) Mkoa wa Arusha Bw. Valence Rutakyamirwa amesema Ofisi ya CAG imeamua kutoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kutokana na umuhimu na mchango wa vyombo vya habari katika usimamizi wa fedha na mali za umma.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kitengo Cha Huduma za Kiufundi (TSSU),Deogratisu Kirama amesititiza kuwa ofisi hiyo imeajiri wataalam na wengine ili kuleta tija zaidi katika ukaguzi na udhibiti wa fedha za umma.
"Katika kudhibiti matumizi sahihi ya fedha za Umma Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) inawataalaam wabobezi 400 Wenye CPA ikiwemo wataalam wengine wenye taaluma mbalimbali nchini."
Pia ameendelea kueleza kuwa ni vema wanahabari wanachambua na kuandika zaidi taarifa za CAG ili kujua matumizi ya fedha za umma au za miradi zimefanya kazi yake ikiwemo miradi isiyotekelezwa katika kuchochea maendeleo na kusisitiza ripoti ya CAG ni muhimu kuchambuliwa na hata kama kunahati safi lakini ukienda chini kunakasoro za sheria ya bajeti na manunuzi.
"CAG ameajiri wataalam wengi ikiwemo wenye CPA ili kuleta tija zaidi katika kaguzi lakini pia tunafanya ukaguzi wa kifanisi ambao ni uwekevu,tija na ufanisi katika maeneo yaliyochaguliwa na sio kwa kila taasisi "
Hata Mkurugenzi wa Huduma za Sheria,Elieshi Saidimu amewataka wanahabari kuandika zaidi taarifa zinazotolewa na CAG ikiwemo kujua sheria,kanuni na taratibu zinazoratibu uendeshaji wa ofisi hiyo sanjari na kuchambua taarifa zinazotolewa na CAG.
Post A Comment: