Na Moreen Rojas,Dodoma.
Katika mwaka wa fedha 2023/24, jumla ya barabara zenye urefu wa km 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo, km 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, km 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa pamoja na mifereji ya mvua km 70.
Aidha, Jumla ya Shilingi Bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za Wilaya.
Taarifa hiyo imetolewa leo 24.8.2023 Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif wakati akizungumza ba waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu na mwelekeo wake katika mwaka wa fedha 2023/24.
Mhandisi Victor,amesema Kati ya fedha hizo, shilingi Bilioni 710.31 ni fedha za ndani na shilingi Bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect.
''Mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi Hadi Mwezi Machi, 2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50''amesema Mahandisi Victor
Pia amebainisha Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Morogoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15.
Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema TARURA imeanzishwa mwaka 2017 lengo likiwa ni kupanua mawanda ya namna ambavyo tutawahudumia Watanzania kwa kuwaboreshea barabara.
Post A Comment: