Na John Walter-Manyara
Wakazi takribani elfu themanini (80,000) wa kata za Maisaka, Bagara na Babati Mjini, wanatarajiwa kunufaika na mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Babati, (BAWASA) kwa shilingi bilioni 1.4.
Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Iddy Msuya, ameieleza kamati ya siasa Babati mjini kuwa mradi huo ambao kwa sasa umefikia 50 ya ujenzi, ulianza mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika Septemba 26 mwaka huu kuwaondolea wananchi adha ya maji.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Babati mjini Elizabeth Marley, ameitaka serikali kuharakisha malipo ili mradi ukamilike kwa muda uliopangwa.
Mkuu wa wilaya ya Babati amesema malipo yatafanywa muda wowote kwa ajili ya mradi huo.
Katika hatua nyingine kama hiyo ya siasa ya chama cha mapinduzi imetembelea miradi mbalimbali ya utekelezaji wa ilani ukiwemo wa ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi kupitia boost ambapo wananchi wanaishukuru serikali kwa kutoa fedha zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya maboresho na upanuzi wa miundombinu.
Katibu wa chama cha Mapinduzi Babati mjini Mohammedi Cholaje amesisitiza kuzingatiwa kwa ubora wa vifaa vinavyotumika ili miradi hiyo idumu.
Post A Comment: