Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Benki Kuu ya Tanzania imeanzisha mfumo mpya  wa (TIPS) Tanzania Instruct Payment System utakao wajumuisha wote wenye mifumo ya miamala kuwa pamoja. 

Hayo yameelezwa na Afisa Mkuu Mwandamizi Mifumo ya Malipo Joyce Njau wakati walipotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba na kwamba mfumo huo utaanza rasmi mwaka huu.

"Mfumo huu utasaidia gharama zingine kupungua vilevile utasaidia kuona data zote za mitandao ya simu". Amesema Bi. Njau
 
Benki Kuu inaanzisha mfumo huo kwa ajili ya kuendelea kuboresha mifumo ya Malipo nchini kwa siku zijazo.

Tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu 1966 hadi katikati mwa  miaka ya 1990, Tanzania ilikua na uchumi hodhi ambapo nyanja nyingi za uchumi zilikua zimemilikiwa na Serikali ambapo wakati huo kulikuwa na Mabenki machache, Miundombinu duni, ikiwemo Barabara, Umeme,na nyanja ya mawasiliano.

Mifumo yote hiyo iliyokuwepo wakati huo ilikua na changamoto mbalimbali ikiwemo upotevu wa fedha kwa namna mbalimbali pale malipo yanapofanyika, Ucheleweshwaji wa malipo hundi zinapotumika kufanya malipo, Kughushi kwa namna mbalimbali hundi zinapotumika katika malipo makubwa.

Benki Kuu pamoja na mafanikio yote na changamoto walizozipata katika kuanzisha mifumo ya malipo nchini inakusudia kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuendelea kuboresha na kusimamia uboreshaji wa mifumo yote ya malipo nchini ili iendelee kuwa madhubuti na yenye ufanisi mkubwa kwa watumiaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: