NA DENİS CHAMBİ.

JESHİ la Polisi mkoa wa Tanga  limefanikiwa kumkamata Swalehe Miraji Ally  mwenye umri wa miaka 38  kwa kosa la kuwaua mke wake  pamoja na shemeji yake kwa kuwakata na mapanga mara mbili kichwani wakati wakiwa shambani kisha kukimbilia mkoani Tabora.  

Akitoa taarifa hiyo leo Augost 17  kwa waandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polisi  mkoa wa Tanga ACP  Almachius Mchunguzi amesema kuwa  mtuhumiwa huyo ambaye ni  fundi ujenzi mkazi wa  Mkanyageni wilayani Muheza  alimuua mkewe   Mwanahawa Hassan (24) na  Sauda Sufian (20)  kisha kukimbilia Tabora lakini jitihada za Polisi zilifanikiwa na kumkamata mtuhumiwa kwaajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha jeshi hilo wilayani Handeni limefanikiwa  kumkamata Rajab  Athuman  mwenye miaka 32 kwa kosa la   kumuua  kwa kumkata kichwa Helena Sila ambapo bado upelelezi unaendelea kufwatia tukio hilo.

Katika taarifa nyingine kamanda Mchunguzi amesema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwatia hatiani watu watano kwa makosa mbalimbali  ambapo  Ally Kilulu  amehukumiwa miaka 15 jela  kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroin gram 1,    Amos Hamis akihukumiwa  miaka 14 jela kwa kosa la kubaka  huku   Halid Yusufu akihukumiwa   miaka mitano jela  kwa kosa la wizi wa mifugo.

Wengine ni  Bakari Mohammed ambaye amehukumiwa  miaka mitano  jela  kwa kosa la kuvunja duka usiku na kuiba huku  Ernest Petro akihukumiwa  kifungo cha miaka 20 jela  kwa makosa ya  kuzini na  Maharimu (ndugu yake) .

Hata hivyo kamanda Mchunguzi amewataka wananchi  mkoani wa Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapoona viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao ili sheria kali dhidi ya wahalifu na uhalifu ziweze kuchukuliwa.

"Jeshi  la Polis linatoa wito kwa wananchi wote mkoani Tanga kuendelea kutoa  ushirikiano  wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi la Polis ili kuzifanyia kazi na kuimarisha hali ya utulivu na amani"

"Wananchi wa mkoa wa Tanga muendelee kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maendeo yenu na kutumia wakaguzi kata wa jeshi la Polisi waliopo katika kata zote  mkoani hapa  katika kuzuia viashiria  vya uhalifu na wahalifu kabla haujatendeka katika maeneo yenu" alisema kamanda ACP Mchunguzi.



Share To:

Post A Comment: