Na,Jusline Marco;Arusha
Kampuni ya Agricom katika maoneshoya Nanenane njiro jijini Arusha imetambulisha zana mpya ya kilimo aina ya KUBOTA yenye horsepower 75 ambayo ina fourwheel na twowheel kwa mara moja ambayo inatofautishwa na trekta nyingine ambazo zipo sokoni.
Akizungumza katika banda la Agricom Afrika kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini jijini Arusha Meneja wa Kanda ya Kati na Kaskazini Bwn.Peter Temu,amesema uwezo wa trekta hiyo ni sawa na uwezo wa kutumia trekta mbili kwa mara moja ambayo inauwezo wa kufanya kazi mahali popote kulingana na aina ya udogo.
Aidha ameongeza kuwa matengemeo yao kama Agricom ni kuwasaidia wakulima wa Kanda ya Kaskazini kuweza kufanya vizuri kwenye kilimo chao ukitengemea trekta hiyo pamoja na kuwa na horsepower 75 ina ubora mkubwa kwenye matumizi ya mafuta ,bei inayouzwa hadi katika upatikanaji wa vipuri .
Vilevile Meneja huyo amewataka wakulima kutarajia kupata faida kutokana na kile wanachokifanya huku akisema kuwa teknolojia hiyo niya japani na inasambazwa na Agricom Afrika pekee ambapo pia hutathimini njia ya kumuwezesha mkulima kuweza kupata faida zaidi kwa kumuinua kutoka katika matumizi ya zana za zamani na kurudi katika matumizi ya zana za kisasa zinazomuwezesha mkulima kupata faida kutokana na kile anachokifanya.
Post A Comment: