NA DENIS CHAMBI, TANGA.
TAASISI ya afya Check kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wa jimbo la Tanga wanatarajia kuzindua kambi maalum ya kupima afya bure kwa wananchi wa kwa siku tano ikiwa ni mpango wa kuitaka na kuihamasisha jamii kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili pale wanapogundulika kuwa na matatizo mbalimbali waweze kupata matibabu ya haraka.
Akizungumza
na waandishi wa habari waziri wa afya ambaye pia ni mbunge wa jimbo la
Tanga Ummy Mwalimu amesema kambi hiyo itkayofanyika kwa muda wa siku
tano kuanzia Augost 21 ambapo jumla ya wananachi 5000 wanatarajiwa kufanyiwa
uchunguzi katika magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu, Saratani ya
tezi dume,saratani ya mlango wa kizazi.
Waziri
Ummy ameongeza kwa kusema kuw magonjwa yatayopimwa ni yale yanayoambukiza na
yasiyoambukizwa na endapo mtu atakutwa na ugonjwa atapatiwa tiba bure na
kwa wale ambao watakuwa na magonjwa yatakayohitaji upasuaji watapatiwa
tiba watakapokuja madaktari bingwa huku akiipongeza bank ya CRDB ambao
ndio wadhamini wakuu wa kambi hiyo.
"Takwimu
inaonesha wapo watu laki mbili ambao hawajajitambua afya zao katika
upimaji wa vvu, tunawashauri na kuwahamasisha watu kupima na kama watu
wote ambao wana maambukizi wangekuwa wanafuata masharti ya kumeza dawa
tunaweza kuutokomeza kabisa" amesema.
"Niwapongeze
sana sana wadau wetu wakubwa CRDB, benki yetu kwa kujitolea na kuunga
mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, katika kufadhili huduma zinazowasaidia wananchi"
amebainisha.
"Sasa, nitoe
wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Tanga kujitokeza, wilaya zote
kujitokeza kuja kupima katika viwanja vya shule ya sekondari ya Usagara,
lengo ni watu 5000 lakini hata tukipata zaidi itakuwa vizuri"
amesisitiza.
Mratibu mkuu
wa Afya check Isack Maro amesema lengo la kuweka kambi mkoani hapa ni
kutaka kuwajengea wananchi tabia ya kupima afya kwa hiyari mara kwa mara
na hii ni mara baada ya kumaliza mkoani Dar es salaam ambapo zaidi ya
wananchi 9324 walifanyiwa vipimo.
"Kitakwimu
watanzania tunatumia gharama kubwa sana kujitibu na mara nyingi ni kwa
sababu tumechelewa kugundua tatizo sasa kampeni hizi zilianzishwa
kuhakikisha kwamba watanzania wanajenga tabia ya kuoenda kupima afya
zao mara kwa mara na hii inaonyesha kuyokana na matukio tunayoyaona
kutokana na hizi kambi ambazo tumezifanya kwa muda mrefu"
"Kwa
sasa hivi ndio tumetoka kumaliza vipimo kwa wakazi wa mkoa wa Dar es
salaam na wilaya zake zote na tukafanikiwa kuwapatia huduma za afya za
bure wananchi takriban 9324 walifanikiwa kupatiwa huduma zote za
kibingwa pamoja na hufuma za kawaida bila kusahau wakapatiwa dawa na
vipimo"
Post A Comment: