Waziri wa kilimo wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Hussein Mohamed Bashe amefanya ziara ya kushtukiza katika wilaya ya Monduli kata ya Mto wa Mbu.
Awali akizunguzma na wanachi katika eneo la kigongoni kijiji cha baraka ambapo ametembelea na kukagua eneo linalotarajiwa kujegwa Soko maalumu la mbogamboga amesema wizara inajipanga kuanza ujenzi wa soko hilo siku za hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Mhe. Bashe ametembelea kata ya majengo kukagua skimu ya umwagiliaji ambapo amekuta ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo mafuriko na ukosefu wa uzio jambo linalosababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Akijibu changamoto hizo amesema kupitia wizara yake ya kilimo wataanza kutatua changamoto ya mafuriko kutoka kata ya Engaruka mpaka Mto wa Mbu kwa kujenga mifereji ya kisasa pamoja na uzio litakalo zuia mifugo kufika katika maeneo ya wakulima.
"Hatua za awali tutakazo chukua ni kusakafia mifereji inayopokea maji na kueleka maji mashambani, lakini kazi kubwa tutakayoifanya katika tangazo atakalotoa Mkurugenzi wa tume ya umwagiliaji ni kutangaza hatua ya mifereji miwili ya kupeleka maji shambani na fensi kwa pamoja" Bashe amesema
"Kazi ya pili atakayo ifanya ni kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwanzia Engaruka ambako ndiko chanzo kwajili ya ku dising mabwawa ya kupokelea Maji ili hayo maji yatumeke huku chini, ninaamini hili bonde lote linaweza kubadilisha maisha ya wanamonduli" Bashe amesema.
Kwa upande wake mweyeji wake, mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Fredrick Lowassa amemshukuru Waziri wa kilimo kwa ujio wake wilayani monduli na kusikiliza changamoto za wakulima na kuahidi kuzitaftia ufumbuzi Mapema.
Lowassa amesema maeneo hayo mawili aliyoyatembelea Waziri wa kilimo, eneo la soko na skim ya wakulima ni miongoni mwa maeneo anayo yatamani kushughulikiwa kwani ni ahadi yake kwa wana Mto wa Mbu wakati akiwania nafasi hiyo ya ubunge.
"Wakati naomba nafasi ya ubunge pale chuo cha ualimu Monduli nilipewa dakika tatu pekee kujieleza lakini nimetumia dakika moja na nusu kuaelezea nitakavyo isaidia Mto wa Mbu kwasababu najua Mto wa Mbu ndio penye mapato kwa wilaya ya Monduli " Lowassa amesema.
Ujio wa ghafla wa Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Mohamed Bashe imewatia matumaini wananchi wa wilaya ya Monduli hasa kata ya Mto wa Mbu kwani imegusia kwa kiasi kikubwa changamoto tajika kwa wanachi hao.
Post A Comment: