NA DENIS CHAMBI, TANGA.
Waziri
wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameridhishwa na
mafunzo kwa vitendo yanayotolewa na kituo cha Sayansi cha Stem Park
kilichopo jijini Tanga akipongeza hatua waliyofikia ambayo inakwenda
kujenga na kuzalisha na kuwaandaa wabunifu na wataalam wa maswala
mbalimbali hapa nchini.
Waziri
Mkenda ametoa pongezi hizo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na
kujionea shughuli zinazofanyika na kituo hicho kinachotoa mafunzo ya
ubunifu kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari
waliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Tanga ambapo amesema kuwa
"Tunajua
kwamba project inspire wanacho kituo kama hiki mkoani Dar es salaam
lakini tutashirikiana nao waanzishe kituo kikubwa mkoani Dodoma na
wabunge nitapenda wakija watembelee pale waone nini kinachoweza
kufanyika na tujenge vituo kama hivi nchi nzima tuanzie na Dodoma
najua haitafikia wanafunzi wote lakini utaanza kuhamasisha na kwenye
mitaala mipya tutanzia na kata"
"Huko
tunakoenda mwalimu anatakiwa kujaribu kuwafikirisha watoto wa kuweza
kufanya uvumbuzi kutokana na ubunifu wao uwepo wa kituo hiki ni muhimu
sana kwaajili ya kuchochea ubunifu kwa vijana wetu kwa sababu vitu
vyote wanavyotengenezea vinapatikana katika mazingira yetu" alisema
Profesa Adolf.
Akizungumza
mkurugenzi wa kituo hicho cha Sayansi teknolojia na Mahesabu (Stem
Park) kilichopo chini ya project inspire Dkt. Lwidiko Mhamilawa alisema
kuwa malengo yao makubwa ni kutaka kuona nchi inakuwa na wanasayansi
mbalimbali wanaozalishwa ndani ya vituo vyao wakiendana na mabadiliko
ya teknolojia ya sasa katika kujenga vijana kuweza kujiajiri mwenyewe
kupitia uwezo wao binafsi.
"Kazi
yetu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawalea watoto kutokana na udadisi
wao wa kiasili wa kisayansi mpaka kuwatengenezea wawe wana sayansi
halisi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujifunza kwa miradi na
kuwaangalia mazingira ya kuhamasa kusoma tangu wakiwa wadogo na kupewa
fursa mbalimbali"
"Nchi
zote zilizoendelea duniani kwa asilimia 60-70 karibia mapato ya ndani
yanayokana na taaluma ya uhandisi , Teknolojia na Mahesabu na Tanzania
ili tuweze kufika huko tunahitaji wana taaluma wengi na ndio maana
tumekuwa tukifanya hivyo kwa miaka nane sasa" alisema Dkt Mhamilawa.
Aliongeza kuwa tangu kituo hicho kilipoanzishwa kwa miaka mitatu zaidi ya wanafunzi 30,000 wa
elimu ya msingi na sokondari wamepata mafunzo na matokeo yamekuwa ni
chanya ikiwa ni pamoja na walimu kupata uzoefu wa namna bora ya
kufundisha masomo ya sayansi kwa njia tofauti tofauti.
"
Kwa hapa Tanga tumechukua wanafunzi wa kutoka jiji zima tangu mwaka
2021 mpaka leo tuna wanafunzi karibu 30,000 wamekuja kutembelea kwenye
kituo na matokeo ni mazuri mpaka sasa ikiwemo walimu ambao wamekuwa
wakija hapa kujifunza namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi na
mahesabu na wamekuwa wakitupa mrejesho hii inaonyesha kwamba hiki kituo
kimekuwa ni msaada kwa walimu kwenye ufundishaji wao" aliongeza
Kwa
upande wake mkurugenzi mkuu wa tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia
"Costec" Dkt Amos Nungu amesema uwepo wa kituo hicho ni njia bora na ya
kipekee katika kuwahamasisha vijana kupenda na kujifunza masomo ya
sayansi hivyo ili kupata wataalam mbalimbali wa baadaye wanaendelea
kuhamasisha na hatimaye nchi nzima kuwepo na vituo vya kufundishia
masomo ya sayansi kwa vitendo.
"Hii
ni project inayohamsisha kujifunza masomo ya sayansi Teknolojia na
Mahesabu kwa ufanisi zaidi kwa wanafunzi kujenga uelewa tunakaribia
kuhamasisha kusudi nchi nzima tuweze kupata vituo kama hivi vya watoto
kujifunza masomo ya sayansi na teknolojia kwa sababu vinasaidia kujenga
umahiri na upenzi wa sayansi kwa watoto wadogo" alisema Dkt Nungu.
Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akiwapongeza wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi kwa vitendo katika kituo cha Stem Park Tanga mara baada ya kufika kituoni hapo katika ziara yake mkoani humo.
Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza jambo katika kituo cha stem park kilichopo jijini Tanga (kulia) kwake ni mkurugenzi wa kituo hicho Dkt.Lwidiko Mhamilawa
Mkurugenzi wa kituo cha Sayansi ,teknolojia na Mahesabu (Stem
Park) kilichopo chini ya project inspire Dkt. Lwidiko Mhamilawa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelewa na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda july 11,2023.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha sayansi , teknolojia na mahesabu ( Stem Park) kilichopo jijini Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati alipotembelea kituoni hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha sayansi , teknolojia na mahesabu ( Stem Park) kilichopo jijini Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati alipotembelea kituoni hapo.
Post A Comment: