Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewapongeza
madakitari na wauguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutokana na
juhudi mbalimbali zinazofanyika katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi huku
akisisitiza weledi na uadilifu katika kazi.
Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua
utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku mbili Mkoani humo.
Waziri Ummy ameridhishwa na juhudi mbalimbali
zinazofanywa na madakitari na wauguzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga katika kuimarisha utoaji wa huduma bora huku akiwakumbusha kufanya
kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za wizara ya Afya.
“Nimefurahi
kuona Hospitali hii kwa sasa inatoa huduma takribani kwa silimia Mia moja hongereni sana kwenye hili nipongeze
sana watumishi mmefanya kazi kubwa nimpongeza Dkt. Luzila na timu yako mmefanya
kazi nzuri tena kwa ubunifu nisidanganye Shinyanga kwakweli nimefurahi na
nimeridhika kwa asilimia Mia moja kama Waziri wenu niseme hamjamwangusha Rais
Samia Suluhu Hassan”.amesema Waziri Ummy
Amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha inakamilisha
ujenzi wa miundombinu yote muhimu katika Hospitali hiyo ikiwemo jingo la mama
na mtoto pamoja na maabara.
Katika taarifa yake mganga mfawidhi wa Hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John amebainisha mafanikio, changamoto
na mikakati mbalimbali ya Hospitali hiyo.
“Kwa sasa huduma
zote za matibabu ya wagongwa wa ndani na wagongwa wa nje zinafanyika katika Hospitali
hii ya rufaa ikiwa ni pamoja na huduma zote za krinick za kibingwa zote,
upasuaji watoto magongwa ya ndani pamoja
na watoto”.
“Kipaumbele
chetu kwa sasa ni kujenga jingo la mama na mtoto, jengo la Maabara, Mochwari,
Famasi na Laundry”.
‘”Uchache
wa miundombinu za majengo ili kuweza kukidhi kutoa huduma zote katika Hospitali
hii ni changamoto kwetu, kuna upungufu wa watumishi kwa asilimia 47, kuharibika
kwa barabara na kutokuwepo kwa Mochware
hii nayo ni changamoto kubwa kwetu”.amesema Dkt. Luzila
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata huduma
katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wamepongeza juhudi mbalimbali za
uboreshaji wa huduma za Afya lakini wameiomba serikali ifanye juhudi za
kuboresha barabara inayotoka mjini Shinyanga kuelekea Hospitali hiyo.
Aidha Waziri Ummy ameahidi kuendelea kushinikiza ili
barabara hiyo iweze kuboreshwa katika kiwango cha lami ambapo amesema serikali
itaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kurahisisha
upatikanaji wa huduma bora za Afya Nchini.
Naye mganga
mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile pamoja na mambo mengine ameahidi
kuendelea kusimamia utoaji wa huduma za Afya.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu emefanya ziara yake ya siku mbili Mkoa wa
Shinyanga ambapo Alhamisi Julai 13,2023 ametembelea na kukagua utoaji wa huduma
za Afya katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na Hospitali ya rufaa ya Mkoa
wa Shinyanga huku akizungumza na watumishi pamoja na wananchi mkoani humo.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akikabidhi
Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto wodi za watoto wachanga mahututi, kwa Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akikabidhi
Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto wodi za watoto wachanga mahututi, kwa Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Hafla ya kukabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto wodi
za watoto wachanga mahututi ikiendelea katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Hafla ya kukabidhi Vifaa Tiba kwa ajili ya watoto wodi
za watoto wachanga mahututi ikiendelea katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Post A Comment: