Mmoja wa Wataalam wa Sekta ya Afya Hospitali ya Mji Babati mkoani Manyara akielezea changamoto walizonazo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi.
...............................................
Na Mwandishi Wetu, Babati
WATAALAM wa Afya wa Hospital ya Mji Babati mkoani Manyara wametoa malalamiko yao kwa Mbunge wa Jimbo la Babati Mji Pauline Gekul kutokana
na changamoto wanazozipitia kwenye masuala
ya kiutumishi.
Wataalam hao wametoa malalamiko hayo baada ya
kukutana na mbunge huyo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya
maendeleo na kusikiliza kero za wananchi, ziara ambayo anaifanya jimbo jimbo
lote baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge la bajeti hivi karibuni.
Baadhi ya malalamiko waliolalamikia ni ufinyu wa
kikokoteo baada ya kustaafu, kutopandishiwa mishahara baada ya kumaliza masomo
Yao pindi wakiwa Kazini pamoja na kucheleweshewa kwa pindi wanapohamishwa vituo
vya kazi.
Hivyo wamemuomba Mbunge huyo kupelekea malalamiko
yao Bungeni ama kwa Waziri husika ili wajue namna ya kutatua changamoto zao.
"Nilikuwa sijui kuhusu changamoto hii
nitazifikisha kwa wahusika naamini ndani ya muda zitafanyiwa kazi kwani ni
jambo la kitaifa," alisema Gekul.
Wakati huo huo wakazi wa Mtaa wa Dawari Kata ya
Bonga wameilalamikia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kutowalipa fidia
zao ndani ya miezi mitatu baada ya kufanya kazi walizopangiwa kufanya ili
kujikimu na kimaisha.
Malalamiko hayo yamekuja mara baada ya Mbunge wa
Jimbo la Babati Mji Pauline Gekul kufanya ziara katika Kata hiyo ikiwa na lengo
la kusikiliza na kutatua Kero za wananchi
Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo Mkuu wa Idara ya TASAF wa Halmashauri ya Mji Babati, Esther alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo lakini malipo yao yameshindwa kukamilika kutokana na baadhi yao kufanya kazi nje na utaratibu na kuwa fedha za ruzuki ziko pale pale kwa wale ambao wamekithi vigezo vya kufanya kazi za kijamii.
Post A Comment: