Na John Walter-Babati


Wananchi wa Kijiji cha Gichameda kata ya Magugu wilaya ya Babati wamesema hawana cha kumlipa Mbunge wao Daniel Sillo kwa kuwa amewafanyia mengi waliyoyahitaji Kwa kwa muda mfupi.

Wamesema awali walikuwa na changamoto ya bara bara na daraja ambapo Mbunge huyo aliwaahidi na sasa wanapita bila shida baada ya kukamilika ambapo Biloni 1.2 imetumika.

Aidha wananchi hao walisema waliomba kupatiwa mashine ya kuchapisha mitihani ambapo ahadi hiyo ameitimiza kwa vitendo.

Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Gichameda Micah Mughuna  amesema mashine hiyo itaondoa usumbufu wa kwenda kuchapisha mitihani mbali na kuokoa  gharama na badala yake itakuwa ikichapishwa shuleni hapo kila itakapohitajika.

Mwalimu Mughuna amesema kwa furaha waliyoipata wameona wamzawadiye Mbunge Mheshimiwa Daniel Sillo shuka (Mgorori) kama kumbukumbu na ishara ya kukubali utendaji wake katika Jimbo la Babati Vijijini.

Sillo amewasihi Wanafunzi wasome kwa bidii wakati serikali na Wazazi wao wanapoendelea kuboresha zaidi miundombinu ya Elimu.

Aidha amewataka wasiige mambo yasiyofaa katika jamii kwa kuwa kila kitu watakipata watakapohitimu masomo.
Katika hatua nyingine amewapongeza walimu kwa kazi Kubwa ya malezi wanayofanya ya kuwalea watoto na kuwaelimisha.
Share To:

Post A Comment: