Imma Msumba ; Arusha
Jumla ya walim 500 wa TEHAMA wamefanikiwa kuhitimu mafunzo ya matumizi ya vishkwambi katika kufundishia huku wakipewa kibarua cha kuzalisha wanasayansi nchini.
Kibarua hicho kimetolewa Mkoani Arusha na naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe wakati akifunga mafunzo ya siku tano ya walim hao waliopatiwa mbinu mpya za matumizi ya Tehama na vishkwambi katika kufundishia.
Alisema kuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika Mafunzo hayo ili kuleta mapinduzi makubwa ya elim hasa katika kuzalisha wanasayansi wengi kuanzia ngazi ya Sekondari watakaokuwa msaada kwa serikali baadae.
"Ulimwengu hauwezi kujengwa bila wanasayansi, na kwa kutambua hilo serikali inakwenda kufanya mapinduzi makubwa ya Elim kupitia utekelezaji wa miradi yake ikiwemo huu wa kuwapatia Mafunzo, sasa nasisitiza muende mkatekeleze kwa vitendo" alisema Prof. Mdoe.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa kuboresha Elim ya Sekondari (SEQUIP,) Dkt Mollel Meigaru alisema kuwa Mafunzo hayo yanayolenga kuwanoa walimu namna bora ya kufundisha masomo ya sayansi kwa kuhusisha na tehama, uko chini ya ufadhili wa benki ya dunia kwa mkopo wa dola milioni 500.
Alisema malengo makuu ya mradi huo ni kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elim ya Sekondari, kuweka mazingira wezeshi ya ujifunzaji kwa wasichana , pia kuwezesha wasichana na wavulana kukamilisha mzinguko wa Elim kwa kupata Elim bora ya Sekondari
"Katika kufikia malengo hayo, mradi pia utajenga miundo mbinu ya shule za sekondari ikiwemo shule 1000 za mchanganyiko na zingine 26 za wasichana za mchepuo wa sayansi kwa mikoa yote Tanzania ambayo Kila shule itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1000" alisema .
Alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamefanikiwa kujengwa shule 232kwenye kata zisizo na shule ya Sekondari nchini ambapo kwa mwaka ujao 2023/2024 wanalenga kujenga shule 214.
Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi Mafunzo ya walimu, Huruma Mageni alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa kuwapatia Mafunzo hayo na kuwataka wanufaika kuhakikisha wanautendea haki Ili kuleta thamani ya fedha.
"Kwa miaka mingi walimu wamlilia Mafunzo na leo serikali imetoa, sasa nendeni mkaisaidie serikali kuona thamani ya fedha hizi kwa kufundisha kwa weledi huku mkitumia ujuzi huu mlioupata katika kuhakikisha mapinduzi makubwa ya elimu yanapatikana"
Mmoja wa walim waliopata mafunzo hayo, mwl James Otieno alisema kuwa Mafunzo hayo yana tija kubwa kwa walim wanufaika na wanafunzi pia watakaoenda kufundishwa kuanzia sasa.
"Itasaidia kuleta ufanisi katika ufundishaji hasa katika silabasi ambazo zilikuwa zinafundishwa zilizopitwa na wakati kutokana na uzoefu wa mwalim lakini sasa Mafunzo yataongeza umahiri katika ufundishaji na wanafunzi pia katika kutembea juu ya yale waliyofundishwa"
Post A Comment: