Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana jijini Dar es Salaam jana Julai 10, 2023 katika mkutano wa siku tatu.
Na Mwandishi Wetu
WAKUU wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi za SADC
wamekutana jana Julai 10, 2023 jijini Dar es Salaam, kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja
ya kuboresha mpango wa manunuzi ya pamoja ya bidhaa za afya kwa nchi za ukanda
wa Kusini mwa Africa-SADC (SPPS).
Washiriki hao pamoja na mambo mengine watajadili namna bora ya kutekeleza mpango wa manunuzi ya pamoja ili kuweza kutekeleza mpango huo kwa ufanisi zaidi na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na mshauri mwelekezi.
Nchi 16 Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo ni wanachama wa mpango huo wa manunuzi ya bidhaa hizo za afya ni Angola, Boswana, Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Seychellers, Msumbiji, Namibia, Afrika ya Kusini, Eswatini, Tanzania , Zambia, Comoros, na Zimbabwe.
Mkutano huo wa siku tatu ulianza jana Julai 10, 2023 na utafikia tamati kesho Julai 12, 2023 kwa wakuu wa taasisi hizo kutembelea Bohari ya Dawa (MSD) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika zikiwamo za uhifadhi wa dawa na vifaa tiba.
Post A Comment: