NA DENIS CHAMBI,  TANGA.

WAUMINI wa dini ya Kiislam wameaswa kupenda kusoma na kufuata maagizo ya mwenyezi Mungu kupitia kitabu cha  Quran tukufu  na sii kupotosha jamii huku wakitakiwa kupenda kufuata kalenda na matukio mbalimbali ambayo ni muhimu kiimani.

Wito huo umetolewa na Sheikh Shafii Mohammed wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ashuraa ,  siku ambayo ni kumbukizi ya kifo cha kichukuu cha mtume 'S,.A.W'  Imamu Houssein aliyeuwawa mwaka wa 61 Hijiria nchini Irak akitetea dini.

"Matukio ya tarehe ni muhimu sana yasomwe ili kujua huko nyuma kulikuwa na nini na kujifunza vizuri uislamu kupitia vitabu vikiwemo tourat, injili,  zaburi hivi vitabu vilikuja kutoka kwa mwenyezi Mungu" alisema Sheikh Shafii.

Akizungumza Sheikh Ally Mwazoa amesema kuwa yapo mengi ya kujigunza kwa waislamu kupitia kifo kwa Imamu Hussein ikiwa ni pamoja na kukemea rushwa ambalo ni adui wa haki na hupelekea athari mbalimbali ambazo ni maumivu kwa wengine pamoja na kumpenda Mungu kuliko kiumbe chochote hapa duniani..

"Kuna mafunzo mengi ambayo twayapata katika tukio la kuuwawa mtukufu al Imamu Houssein moja ya funzo ni kukemea suala la rushwa ambalo ni adui wa haki na inaathiri jamii kubwa ya watu, lakini fundisho lingine ambalo tunapata ni kuzidi kujipendekeza kwa viumbe usizidi kujipendekeza kwa  mwenyezi Mungu aliyekuumba" alisema Sheikh Mwazoa.

Kwa upande wake mwalimu Madrasa kutoka taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania tawi la Tanga , Shehat Athuman amewataka waumini kutenda na kuishi kadiri ya mapenzi yake Mungu wakiwa ni wafuasi kamili wa Mtume S.A.W.

"Nawausia pamoja na kuiusia nafsi yangu turudini na tusome historia tuangalie bwana Mtumbe S.A.W aliishi vipi katika uislamu je hayabtunayoyafanya ni yale mtume aliyotuusia na anayoyataka na mwenyezi Mungu ameyaridhia










 lakini ukisoma na ukaelewa vizuri huwezi kwenda na kutenda kinyume na yale ambayo mwenyezi Mungu ametuusia" alisema Shehat Athuman.
Share To:

Post A Comment: