Julieth Ngarabali 


Wadau mbalimbali 589  kutoka sekta ya kilimo ,uvuvi na ufugaji  wamedhibitisha kushiriki kwenye maonyesho ya 30 ya nane nane  Kanda ya mashariki  ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 22 ikilinganishwa na wadau 476 walioshiriki mwaka jana.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Mkoani Morogoro  Agosti mosi na mgeni rasmi ni Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda   na kwamba inahusisha mikoa minne ya Dar esalaam, Morogoro, Tanga na Pwani 

Ikumbukwe kwamba Waziri mstaafu Pinda na yeye ni mkulima,mfugaji na mvuvi mzuri huko katika makazi yake.

Akitoa taarifa ya maonyesho hayo kwa niaba ya wakuu wa mikoa hiyo minne,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge  amesema washiriki hao wamejiandaa  katika teknolojia mbalimbali  za kilimo, mbegu bora za kilimo, njia bora za kilimo,njia bora za matumizi ya mbolea na, matumizi ya maji kidogo,

Nitoe rai kwa Wananchi kutoka katika mikoa hiyo minne kuja kwa wingi kutembelea maonyesho haya kwa sababu watapata  fursa ya kuona teknolojia mbalimbali za kisasa katika kilimo,ufugaji na uvuvi  "amesema Kunenge na kuongeza

" Na hii hasa ndio lengo la maonyesho yetu ya nane nane sisi Kanda ya mashariki tumejiwekea malengo kwamba lazima yale yanayoonekana katika nane nane yaweze kuakisi katika maeneo yetu" amesema

Kauli mbiu itakayobeba maonyesho hayo ni vijana na wanawake ni msingi imara  wa mifumo endelevu ya chakula .

"Kauli mbiu hii inatambua mchango wa vijana na wanawake katika kuhakikisha suala zima la uzalishaji , uhifadhi ,usalama wa chakula na matumizi ya chakula na vile vile inaendana na jitihada za Rais awamu ya sita kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji wa chakula katika nchi yetu na hivyo kulisha bara la Afrika na Dunia" amesema Kunenge

Share To:

Post A Comment: