DENIS CHAMBI, TANGA.
ZAIDI ya wanafunzi 60 wa shule za sekondari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameshiriki kikamilifu kongamano la saba la sayansi na Teknolojia lililoandaliwa na kituo cha sayansi Cha Stem Park chini project Inspire wakifunzu na kuonyesha umahiri wao katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia sayansi ,technolojia, uhandisi na hisabati.
Akifunga kongamano hilo la
saba mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dr. Sipora
Liana ameipongeza shirika la botna foundation ambao ni wafadhili wa
miradi mbalimbali inayotekelezwa jijini humo ikiwemo kituo cha Stem
Park huku walimu wanaowafundisha vijana na wanafunzi akiwataka mbali na
elimu kuwafundisha pia maadili mema.
"Tunatambua
mchango mkubwa sana wa botna foundation ni mengi sana wametusaidia
katika nyanja ya kielimu kijamii na hata afya pia wametoa Madawati ya
shule za msingi Milion 286.3 , Mambo ya usalama barabarani wametoa
million 442.5 , wamejengea uwezo kiuchumi vijana million 434.9 hii
miradi yote ni maendeleo makubwa ndani ya jiji la Tanga kwaajili ya
wananchi" alisema Dkt. Liana
Akizungumza
na wanafunzi hao amewataka kusimamia ndoto zao kujikita kimasomo zaidi
kuhakikisha zinafanikiwa akiwataka kujiepusha na tamaa maswala ya
ukatili ambayo yataweza kuharibu malengo yao waliyojiwekea huku
akiipongeza kituo cha Stem Park kwa uwezeshaji huo kwa vijana.
"
jilindeni vijana na jitunzeni msome kwa bidii ili mfikie lengo wazazi
wenu wafurahi na mtapata baraka nyingi kwa wazazi , mambo ya uzinzi ,
ukahaba ushoga , usagaji achaneni nayo zingatieni masomo yenu mfikie
malengo yenu nawatakia kila la kheri" alisema Dkt. Liana
Mratibu
wa makongamano hayo Dr. Isaya Ipyana alisema kuwa wanafunzi hao
ambao waliweka kambi kwa zaidi ya siku 5 katika kituo cha Stem Park
wamekuwa wakiwaelekeza namna gani ya kukabiliana na changamoto ya
mabadiliko ya tabia nchi pindi wanapokuwa mashuleni na hata baada ya
kumaliza elimu yao ambapo wataweza kutumia sayansi Teknolojia uhandisi
na mahesabu ambayo walifundishwa kwa nadharia darasani na hivyo kufanya
kwa vitendo hatua ambayo wakifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
"Kongamano
la mwaka huu tulikuwa tumelenga hasa kwenye changamoto ya mabadiliko ya
tabianchi jinsi gani ambavyo watatumia sayansi uhandisi na mahesabu
kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwahiyo kuanzia tarehe 26
mpaka 30 June wanafunzi kutoka mkoa 10 ya Tanzania nzima waliokuwa
pamoja kukaa chini na kuutafuta njia mbadala ambazo wanaweza kuzitumia "
alisema
" Wapo ambao
waliweza kutengeneza ni ndege nyuki ( drones), wapo ambao waliweza
kutengeneza mitambo kwaajili ya gas, kwahiyo nia kubwa ni kuhakikisha
Yale ambayo waliweza kujifunza darasani kwa nadharia wajifunze kwa
vitendo hapa na tunashukuru kwamba wamefanikiwa" alisema Ipyana.
Alisema
lengo lao kuu hasa ni kuwaandaa watoto na vijana ambao watakiwa Ni
wabunifu na kuweza kutatua changamoto mbalimbali kwa kupitia yale
amabayo walishayasoma darasani ikiwemo Yale ambayo yanawazunguka katika
mazingira wanayoishi.
"Dhima
kubwa Ni kuhakikisha tunatengeneza vijana ambao ni wabunifu na kuweza
kutatua changamoto mbalimbali kwa kupitia Yale ambayo wanayasoma
darasani kwahiyo mafunzo haha yanahakikisha tunapata vijana wabunifu
ambapo pia Wana uwezo was kufikiria zaidi ili kuweza kutatua changamoto
mbalimbali ikiwemo tabia nchi na zile ambazo zinawazunguka kwenye jamii
yao" aliongeza Dk. Ipyana.
Akizungumza
kwaniaba ya Botna Foundation Mbogolo Philoteus alisema shirika hilo
linaamini kumuandaa kijana katika karne ya sasa na ijayo kwaajili ya
kuingia kwenye soko la kiushindani hatua ambayo inasaidia kujiepusha
kujiingiza katika mmomonyoko wa maadili na makundi maovu ambayo yanaweza
kumfanya kutokutimiza ndoto zake kielimu , kijamii kisaiasa na nyanja
mbalimbali.
Baadhi ya
wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Nabiha Kassim na Innocent
Richard wamekishukuru kituo cha Stem Park kwa elimu waliyoipata ambayo
mbali na kwenda kuitumia baada ya kumaliza masomo itakuwa ni fursa ya
kuwatengenezea ajira ya baadaye.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari Philter Federal ya Zanzibar, Rashid Said kuhusu utambuzi wa mimea ikiwa ni njia moja wapo ya utunzaji wa mazingira na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mwanafunzi Grace Daniel (kulia) akitoa maelezo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana kuhusu kubaini usalama na hatari karibu na mazingira ya binadamu kutokana na mtambo walioutengeneza katika kituo cha sayansi cha Stem Park wakati wa maadhimisho ya wiki ya sayansi Afrika
Post A Comment: